I hope these tips zitawasaidia, kumbuka tuna nywele na genes tofauti, wengine wakiwa kwenye baridi nywele zinakua zaidi ila wengine ndio nywele haikui
TIPS
🍃Usioshe nywele mara kwa mara, unaweza kuwa na utaratibu wa kuosha nywele mara 2 au 3 tu kwa mwezi, na hapa utatumia shampoo.
-Nasema hivi kwa kuwa kuna wengine bado wanatumia maji ya chumvi au shampoo zenye sulfate, hii inaondoa mafuta yote na unyevu wote nywele inakua kavu mno, hii ni tofauti na kuspray mara kwa mara.
🍃Tumia maji ya uvuguvugu kuspray nywele zako au hata kama unatumia majani ya mpera warm the water.
-Tunafanya hivi kwa sababu hair pores zikipata ubaridi zinajifunga so kwa hali ya kawaida zinahitaji joto ili zijifungue na ww keep in mind kua joto ni muhimu kwa nywele na baridi ikipita pores zinajifunga and you are good to go.
-Usipake mafuta yaliyoganda au ya mgando (hapa najua kuna wengine ata mafuta ya nazi yanaganda) hayasaidii muhimu mafuta yaingie kwenye ngozi, sasa ukitaka kupaka mafuta chemsha maji weka kwenye bakuli halafu weka kopo la mafuta yako au mafuta kdg ambayo unataka kutumia then ndio upake.
-Steaming ni muhimu kwa kuwa ni njia pekee ambayo nywele zako zinapata nutrients; na hapa kwenye steaming joto linahitajika ili pores zako ziweze kufunguka.
-Na hapa hakuna njia nyingine zaidi ya kwenda saloon uingie kwenye steamer au kama una blow dryer nyumbani bas pitisha kwa juu ili joto liingie na baada ya hapo utaosha.
Kumbuka kuanza na maji ya uvuguvugu.
🍃Unahitaji good sealing oil au cream au butter (shea butter)
Kazi ya sealing oil ni kuzuia nywele au ngozi isipate ukavu kwa haraka, ile moisturizer uliyospray baadae juu isikauke kwa haraka.
-When your hair is well sealed hata upepo ukipita utaanza kuaffect mafuta kwanza na sio nywele au ngozi/scalp direct.
Tuesday, August 27, 2019
Sunday, August 25, 2019
4. VITU MUHIMU KATIKA UTUNZAJI WA NYWELE
5. Conditioner (Antie Jackies) na Deep conditioner (Cantu)
Hii ni moja ya product muhimu sana katika kutunza nywele iwe ni za asili au zenye dawa. Kama ambavyo mwili unajitaji chakula cha aina tofauti tofauti vivyo hivyo kwenye nywele pia. Deep conditioner na conditioner ni chakula cha nywele ambacho kinazifanya nywele ziweze kukua vizuri zikiwa zina afya na nzuri.
Conditioner inaoshwa baada ya muda mfupi sana (chini ya dakika 20) lakini deep conditioner inakaa muda mrefu kwenye nywele, kuanzia dakika 30 na kuendelea. Pia ni vizuri kutumia moisturizer deep conditioner ili unyevu wa nywele usipotee kirahisi.
6. Leave in conditioner
Hizi zipo ambazo ni za kutengeneza mwenyewe nyumbani mfano Rojo ya bamia au aloevera(nitaelekeza jinsi ya kutengeneza huko mbeleni) na za kununua (za kiwandani) mfano Antie Jackie’s na Cantu Leave in conditioner. Hii inatumika baada ya kuosha nywele na kupaka mafuta ili kuzipa nywele unyevu.
7. Butters/Hair cream (mfano shea butter)
Hizi zinapakwa baada ya kupaka leave in conditioner pamoja na mafuta ya nywele ili kuseal in moisture (au unyevu) usitoke kirahisi. Hii inafuata mpangilio ufuatao (LOC Method yaani baada ya kuosha nywele unapaka Leave in conditioner (L) halafu Oil (Mafuta ya nywele) mwisho Cream au butter (C).
8. Kitamba cha cotton/microfiber towel
Hiki ni kitambaa maalum kwa ajili ya kukaushia nywele, kinakua na uwezo wa kufyonza maji kirahisi bila kukata au kusumbua nywele. Pia unaweza tumia Tshirt ya cotton (chochote unachoweza afford kirahisi). Usijaribu kutumia taulo la kawaida maana linakata nywele wala usitumie dryer mara kwa mara maana nywele inakua dhaifu na ni rahisi kukatika.
9. Steamer (Deep conditioning cap)
Hii ni moja ya product muhimu sana katika kutunza nywele iwe ni za asili au zenye dawa. Kama ambavyo mwili unajitaji chakula cha aina tofauti tofauti vivyo hivyo kwenye nywele pia. Deep conditioner na conditioner ni chakula cha nywele ambacho kinazifanya nywele ziweze kukua vizuri zikiwa zina afya na nzuri.
Conditioner inaoshwa baada ya muda mfupi sana (chini ya dakika 20) lakini deep conditioner inakaa muda mrefu kwenye nywele, kuanzia dakika 30 na kuendelea. Pia ni vizuri kutumia moisturizer deep conditioner ili unyevu wa nywele usipotee kirahisi.
6. Leave in conditioner
Hizi zipo ambazo ni za kutengeneza mwenyewe nyumbani mfano Rojo ya bamia au aloevera(nitaelekeza jinsi ya kutengeneza huko mbeleni) na za kununua (za kiwandani) mfano Antie Jackie’s na Cantu Leave in conditioner. Hii inatumika baada ya kuosha nywele na kupaka mafuta ili kuzipa nywele unyevu.
7. Butters/Hair cream (mfano shea butter)
Hizi zinapakwa baada ya kupaka leave in conditioner pamoja na mafuta ya nywele ili kuseal in moisture (au unyevu) usitoke kirahisi. Hii inafuata mpangilio ufuatao (LOC Method yaani baada ya kuosha nywele unapaka Leave in conditioner (L) halafu Oil (Mafuta ya nywele) mwisho Cream au butter (C).
8. Kitamba cha cotton/microfiber towel
Hiki ni kitambaa maalum kwa ajili ya kukaushia nywele, kinakua na uwezo wa kufyonza maji kirahisi bila kukata au kusumbua nywele. Pia unaweza tumia Tshirt ya cotton (chochote unachoweza afford kirahisi). Usijaribu kutumia taulo la kawaida maana linakata nywele wala usitumie dryer mara kwa mara maana nywele inakua dhaifu na ni rahisi kukatika.
9. Steamer (Deep conditioning cap)
Hiki ni kifaa maalumu kwa ajili ya kuzipa nywele joto wakati wa kufanya deep conditioning au kwa lugha iliyozoeleka ni Steaming. Hii ni muhimu kwa sababu steaming yako itaingia kwenye nywele vizuri na kwa haraka zaidi.
Saturday, August 24, 2019
3. VITU MUHIMU KATIKA UTUNZAJI WA NYWELE
1.Sulfate and salts free shampoo (Antie Jackie’s na Cantu shampoos) na Co-wash (Antie Jackies)
3. Spray bottle na Kofia ya satini kwa ajili ya kulalia
4.Scalp messager and cleaner (brash ya kusugulia ngozi ya kichwa)
Thursday, August 22, 2019
2. KITU GANI KINAFANYA NYWELE ZISIKUE AU ZIKATIKE? NA NINI UFANYE KUONDOKANA NA HILO TATZO?
Tuangalie kwanza matatizo ambayo ambayo wengi wetu imekuwa changamoto hadi kufikia hatua ya kukata tamaa, kunyoa nywele au kuzichoka.
Vitu ambavyo hufanya nywele kukatika
💚Kuwa na ratiba mbaya katika kuzihudumia nywele zetu,hapa watu wengi tumeshindwa tunawezaje kupanga ratiba ya kutunza nywele, kuanzia kuosha,kuzipa unyevu,bidhaa nzuri za kutumia ambazo hazina kemikali (Bad products lead to damaged hair).
Moto wa drier
Overdose heat inasababisha nywele kukatika hasa kwa wale ambao kila week lazima aende kublowdry nywele,lazima aende kupass nywele zake,..Kuwa na nywele zenye afya kunahitaji kuacha kabis matumizi ya moto,moto hukata nywele,kuzifanya dhaifu na kupelekea kuwa nyepes(Wenye nywele za asili),Hata wenye dawa ukipunguza matumizi ya moto utaipenda na kufurahia nywele zako.
Misuko inayopelekea nywele kukatika,
Wote tunajua kuna misuko sio rafiki kwa nywele zetu,kukazwa au kuvutwa hupelekea nywele kukatika hvyo kuacha kukua kabisa,Epuka mitindo kinga migumu kwa nywele zako
Chakula
Panga ratiba ya vyakula vyako vyenye kurutubisha mwil na nywele zako,kunywa maji angalau glass 8 kwa siku.
Kuzipa nywele unyevu
Hii ni muhimu sana kila mtu lazima aitie akilini,nywele kavu hukatika na nywele kavu hutokana na kutokuwa na unyevu,zipe nywele unyevu angalau mara tatu kwa week, seal in moisture (paka vitu ambavyo vitaweza kuweka unyevu ukae muda mrefu kama vile shea butter au Black castor oil) .unaweza tumia njia ya Spray bottle kuweka maji,leave in conditioner,mafuta ya asili au hata maji ya mpera kiasi na ukanyunyizia nywele zako,unaweza tembea nayo hyo chupa maana ni ndogo tu unaweza weka kwenye handbag iwe kama dawa,asubuhi mchana na usiku😀.
ITAENDELEA....
Wednesday, August 21, 2019
1. SIRI ZA UTUNZAJI WA NYWELE
NJIA 10 ZA KUFANYA NYWELE ZAKO ZIWE ZA KUVUTIA NA ZENYE AFYA.
kuna vitu vingi vinavyoweza kufanya nywele zako zikakosa afya na mvuto, vitu kama vumbi, upepo, mvua, jua, maji na madawa tunayoweka kwenye nywele zetu pamoja na vyakula tunavyokula ni chanzo kikuu cha nywele zetu kuharibika na kukosa afya na mvuto. leo nimekuletea vidokezo vichache vya jinsi ya kutunza nywele zako.
1.kata ncha za nywele zako
Kukata ncha za nywele zako kunasaidia kufanya nywele zako kujizaa upya, mara nyingi seli katika ncha za nywele hufa. seli zinapokufa huzuia nywele zinazozaliwa kustawi vyema na hivyo kuzifanya nywele zako kukosa afya. japo wanawake wengi huwa hawapendi kukata ncha za nywele zao wakihofia nywele zao kuonekana fupi. lakini ukweli ni kwamba unapokata ncha za nywele zako unasaidia nywele zako kupata nafasi ya kukua vizuri na kuwa zenye afya nzuri na kuvutia.
2.Osha nywele zako angalau mara moja kwa wiki
Kuosha nywele zako angalau mara moja kwa wiki kutasaidia kuzifanya nywele zako ziwe na afya. hata kama uko busy sana basi jitahidi isipite wiki mbili bila kuosha nywele zako.
3.tumia shampoo inayoendana na nywele zako
Tumia shampoo inayoendana na nywele zako, kuna nywele za aina tofauti; kuna nywele kavu, zenye mafuta, mchanganyiko, na pia kuna nywele nyepesi, laini, ngumu na nzito. zipo aina tofauti za shampoo zinazoendana na aina ya nywele zilizopo , hivyo basi ni vyema unapotaka kuosha nywele ukajua ni aina gani ya shampoo utumie, pia mwenye conditioner napo unatakiwa kufanya hivyo hivyo.
4.Zipe nywele nafasi
Nywele nazo huitaji nafasi,kuchana nywele kila siku, kuzipaka nywele jelly kila siku, kuzichana mitindo tofauti, kuziwekea gundi na mafuta tofauti tofauti huzifanya nywele zako zichoke na kukosa afya. hivyo unatakiwa mara moja moja unazipa nywele zako nafasi ya kupumzika. zipumzishe nywele zako kwa kusuka mtindo ya kawaida au rasta za mabutu.
5.usichane nywele kwa nguvu zikiwa mbichi.
Jaribu kuzichana nywele kwa chanuo kubwa, au jaribu kuziacha mpaka zikauke ndo uzichane. unapochana nywele mbichi tumia kitana kikubwa na chana taratibu ukianzia nyuma kuja mbele. kuchana nywele zikiwa mbichi bila kufuata utaratibu kutafanya nywele zako zikatike na ziharibike.
6.zilinde nywele zako unapokuwa unaogelea
Unapokua unaogelea baharini au kwenye sehem ya kuogelea, jaribu kuzifunika nywele zako au zipake mafuta ya kuzui zisiharibike na maji, na unapotoka kuogelea zisafishe nywele zako kwa maji safi na uzikaushe.
7.kula vyakula venye protein na matunda
Kula vyakula venye protein na matunda kutasaidia kuimalisha afya ya nywele zako na kuzifanya ziwe nzuri na za kuvutia.
8.Zifunge nywele zako kabla ya kulala
unapotaka kulala hakikisha unazifunga nywele zako, unaweza kuzisuka mabutu au kuzifunga vizuri na kuzibana. kulala huku ukiwa umeziachia nywele zako hufanya nywele zikatike na kuharibika
9.Tumia mafuta asili
Badala ya kutumia mafuta yenye kemikali nyingi kutoka viwandani, jaribu kutumia mafuta ya asili kutunza nywele zako. Tumia mafuta kama ya nazi au parachichi au mnyonyo kupaka nywele zako.
10.zilinde nywele zako na jua
Wakati utakapokuwa unaelekea kwenye sehemu yenye jua kali, vumbi au upepo. zilinde nywele zako kwa kuzifunika na kofia, scarf au mtandio. pia unaweza kuzipaka sunscreen.
Subscribe to:
Posts (Atom)