Friday, October 25, 2019

29. FAHAMU ZAIDI KUHUSU 4C HAIR TYPE (KIPILIPILI)

Leo tuangalie tabia ya nywele hizo na unachotakiwa kufanya ili kupata matokeo mazuri.
1. Kipilipili
2. Ngumu na nzito
3. Zinajaa sana
4. Zina coils/hair strands zimebanana sana ndio maana nywele zinashikana sana
5. Ina shrink sana (kunywea sana) zaidi ya 70% ya nywele ya kawaida
6. Haina mawimbi hata umwagie maji (labda usuke twists na bantu knots)
7. Ina density kubwa na kujaa sana
8. Ukitaka inyooke na kuwa nzuri suka nywele za uzi au twists mara kwa mara
9.  Hii nywele ni imara sana hivyo inaweza kusukwa au kuwa styled tofauti tofauti na bado ikapendeza bila kukatika
10. Hii ni nywele ambayo inapoteza unyevu kirahs sana hivyo kuipa unyevu inabidi iwe mara kwa mara, pia kuzingatia LOC, LCO methods na variations zake (zitaelezewa kwenye post inatofuata) pamoja na kutumia most of water based products ili kuifanya iwe hydrated most of the times.

NB. Kumbuka mafuta (iwe castor oil, mafuta ya nazi, olive oil n.k) hayawezi kuzipa nywele unyevu na hazina maji pia..sana sana zinaongeza ukavu kwenye nywele.

11. Tumia sana steaming ya bamia, leave in conditioner ya bamia au aloevera products utazipenda nywele zako na zitakua laini.
12. Zingatia sana kudetangle nywele kiusahihi na inaweza chukua muda kuwa straight au kuwa na nafasi kwa sababu zinakua zimejaa.
13. Usitumie moto kabisa iwe kukausha, kunyoosha au kustyle.
14. Panga ratiba ya kutunza nywele zako bila kusahau kuzipa unyevu kila siku
15. Ijue aina ya nywele zako, itunze kwa usahihi na uipende jinsi ilivyo lazima upate matokeo chanya.❤️❤️❤️

Monday, October 14, 2019

28. TOFAUTI KATI YA MBA (DANDRUFF) NA NGOZI KAVU (DRY SCALP)*

TOFAUTI KATI YA MBA (DANDRUFF) NA NGOZI KAVU (DRY SCALP)
Mba/dandruff unasababishwa na mafuta mengi kwenye nywele (sebum) hasa ya mgando n.k (zipo kwenye somo la mba No. 24) lakini Ngozi kavu (dry scalp) ni ile hali ya ngozi kutokua na unyevu unyevu na inasababishwa na kutokuipa ngozi yako ya kichwa unyevu wa kutosha na muda inapotakiwa.

UTAJUAJE KAMA UNA MBA AU NGOZI KAVU?
Mba unaonekana kabisa kama particles ndogo ndogo (unaonekana kabisa kwa macho) na muda mwingine hadi vidonda lakini ukavu wa ngozi unaweza kusense kwa kushika na kunakua kama imepasuka na hii husababisha nywele zisikue au kudumaa LAKINI vyote viwili vinatambulishwa kwa;
-ngozi ya kichwa kuuma au kuwasha
-unaweza kuwa huna mba ila unawashwa (hiyo ni ukavu wa scalp)

UKAVU WA NGOZI YA KICHWA
Kwanza inafaa ufahamu ni nini kinacho kusababishia nywele zako kuwa kavu , na kuanza kukatika katika, mara nyingi nywele kuwa kavu inaweza kutokana na sababu mbalimbali. Hapa kuna machache, na kipi unachoweza kufanya ili kurejesha unyevu katika nywele zako kavu:

VISABABISHI VYA UKAVU KWENYE NGOZI YA KICHWA
☘kutumia vifaa vyenye joto kali kukaushia nywele (hair dryers) , vinaweza kusababisha nywele kuwa kavu.
☘Kuosha nweyele zako mara kwa mara kwa shampoo (Overwashing) bila kuwa na tahadhari kama vile kutumia leave in conditioners na conditioners.
☘kuachia nywele zako kwa muda mrefu kwenye mwanga wa jua,upepo
☘kutumia maji ya chumvi kwa muda mrefu kuosha nywele zako kunaweza kusababisha ukavu wa nywele pia.
☘kutumia chemicals hatari kwa nywele (viambata sumu) mara kwa mara husababisha nywele kuwa kavu.
☘kutumia brash mbaya au styles mbaya ya uchanaji nywele pia husababisha kupoteza unyevunyevu wa nywele na hivyo kufanya nywele kuwa kavu.
☘kutokuficha ncha kwenye mitindo ya nywele

NINI  CHA KUFANYA KUKINGA NYWELE ZAKO ZISIWE KAVU
☘Usitumie shampoo kila mara kuosha nywele zako, kila kitu kizuri ukikitumia kwa wingi kupita kiasi kinakua na madhara hapa jaribu kupangilia angalau siku mbili mbili au zaidi maan hata kutumia shampoo kwa wingi zaidi ina leta madhara, kitaalamu inashauriwa osha nywele zako co-wash angalau mara mbili kwa mwezi na mara mbili hadi tatu kwa mwezi kwa kutumia shampoo
☘Tumia shampoo nzuri inayoendana na nywele zako, hapa yakupasa utambue una aina gani ya nywele na je, ni shampoo ipi ianakufaa zaidi? usitegemee shampoo za saloon ni vyema hata ukienda saloon ukaenda na shampoo yako mkononi kwani saloon nyingine hata shampoo wanachanganya na maji, usiende tu saloon ukakubali kuoshwa hata kwa shampoo usizozifahamu nyingine sio shampoo kabisa
☘Vaa kofia laini au kitambaa ulalapo, jenga mazoea ya kuvaa kofia laini ya kulalia ili kutunza unyevu nyevu wa nywele zako unapolala bila kuwa na kofia au kitambaa unaweza usababisha nywele kuvurugika na wakati mwingine hupoteza unyevu wake taratibu na huweza kusababisha kuwa na ukavu
☘Punguza mionzi ya kunyooshea nywele zako, siku ukitaka kubadili muonekano au ur hair style ukaamua kuzichoma/kusipasi au kunyoosha nywele zako kwa kutumia moto au umeme…unashauriwa kupunguza temperature au kutumia kinga (mafuta maalum) ambayo inafanya nywele zako zisipate damage wakati ya kuzinyoosha hii itakusaidia kutunza moisture sambamba na kupunguza ukatikaji wa nywele zako
☘Tumia Moisturizer/Vilainishi Vya Nywele mara kwa mara, Hakikisha unatumia moisturizer kila siku Wengine hawafanyi kila siku. Inategemea na aina za nywele ulizonazo. Wakati wa kuweka moisturizer,hakikisha unapaka kila mahali haswa kwenye ncha za nywele zako(split ends). Mara nyingi huwa tunazisahau zile za juu. Badala yake wengi tunapaka zaidi kwenye ngozi ya kichwa tu. Ndio maana huwa inasisitizwa kuzikata zile split ends kwa sababu huwa zimekauka na kuwa dhaifu.

Wednesday, October 2, 2019

27. LOC METHOD

Leo tujifunze au  tujikumbushie njia mojawapo ya  kutunza au kuhifadhi unyevu kwenye nywele ijulikanayo kama LOC Method - L= Liquid/Leave in conditioner, O = Oil na C=Cream kama picha inavoonesha.

🧚‍♀️LIQUID  mara nyingi inakua ni maji au water based leave in conditioner ambayo ndio unaanza kupaka kwenye nywele zako ili kufungua pores. Pendelea kutumia spray bottle kwan inafanya maji yapenetrate vizuri kuanzia kwenye ncha za nywele mpaka kwenye ngozi. Nywele kikawaida inahitaji moisture au unyevunyevu ili isikatike na unyevu huo hupelekea kuwepo kwa blood circulation sehemu hisia ili nywele ziweze kuota vizuri

🧚‍♀️Baada ya kuspray nywele zako unakuja kwenye step ya pili ambayo ni OIL, hapa unataka mafuta ya maji kama coconut oil, olive oil, jojoba oil, castor oil au hair serum yoyote unampenda kutumia ila iwe katika hali ya kimiminika au liquid form. Oil inasaidia kulock in moisture baada ya kuzispray nywele  zako maji au leave in conditioner au mixer ya hivyo viwili.

⚡️✨Kuna watu wanakimbilia step ya pili ya kupaka mafuta na kuacha step ya kwanza kuspray nywele maji na hapa ndipo watu wengi hukosea na ndio maana ukavu wa nywele zao hauishi,  mtu anaexperience nywele kuwa kavu kila siku pamoja na kuwa anapaka mafuta kila siku na ya kila aina ila nywele bado kavu. Hiyo ni kwa sababu ya kuruka step ya kwanza ambayo hutoa nywele katika hali ya ukavu na kukimbilia step ya kupaka mafuta. Mafuta pekee hawawezi kufanya nywele zako kutokuwa kavu. (Take note kwenye hizo step mbili ni muhimu sana na zifanywe kwa kufuatana).

πŸ”₯Na step ya mwisho ni CREAM. Baada ya kuspray nywele zako, ukapaka mafuta ya kimiminika tena hakikisha unapaka kwenye ngozi vizuri mpaka nywele juu kabisa kwenye ncha ndio unakuja kwenye step ya tatu na ya mwishop ya kupaka hair cream. Hair cream inasaidia kuseal in moisture yaan kuhifadhi nywele iwe katika hali ya unyevu unyevu  cream ina boost hair growth na pia insect kama hair protection dhidi ya jua, mvua, tupelo na kitu chochote ambacho kinaweza kuaffect nywele zako. Na cream nzuri hapa kwa nywele zako ni Shea butter au Heavy Jamaican Black castor oil (Castor oil nzito) ila ni vizuri kutumia shea butter coz ni nzito zaidi na ina vitamins nyingi sana za kupost hair growth na kulinda nywele na pia kufanya nywele zako zisiwe kavu kirahisi.