Sunday, December 15, 2019

50. MAFUTA MAZURI YA NYWELE AINA ZOTE

Watu wengi wamekua wakihangaika kutafuta mafuta mazuri yatakayoweza kukuza nywele zao kiusahihi na bila madhara yoyote, lakini wengi wamekua wakiangukia katika mikono ya watu ambao hawana ujuzi wa kutosha kuhusu mafuta na matunzo ya nywele in general, kwa hiyo wamekua wakipata mafuta yenye kemikali kali au mafuta makali; kitu ambacho kinawapelekea kutopata matokeo ambayo wanayataka au matokeo wanayoyataka yakachelewa sana.

Sasa leo tuomgelee mafuta ya aina tatu ambayo ni Natural, mazuri sana kwa nywele za aina yote na yatakupa matokeo mazuri ndani ya muda mfupi.

AINA YA KWANZA: MAFUTA YA PARACHICHI (AVOCADO OIL)


Mafuta ya Parachichi yana virutubisho vingi sana kama vile Vitamin A, B, D na E, Protein, Iron (madini chuma), Magnessium, nk ambavyo husaidia sana katika kukuza nywele. Mafuta ya parachichi pia hurekebisha nywele zilizokatika, yanalainishabna kung’arisha nywele na pia hulinda nywele dhidi ya miale mikali, kudhurika na kuungua na jua kali.
NB: Unaweza kuchanganya mafuta ya parachichi kidogo na shampoo wakati unaosha nywele zako ili kuzuia nywele kuwa kavu na kuretain mafuta ya asili (natural oil) kwenye nywele.

AINA YA PILI: MAFUTA YA MNYONYO (CASTOR OIL)
Mafuta haya yana virutubisho vingi pia kama vile vitamin E, protein kwa wingi nk ambavyo husaidia kukuza nywele vizuri zaidi na kuziepusha na kukatika katika. Haya ni mafuta mazuri sana ambayo yanatumiwa kwa nywele za aina zote, yana faida nyingi sana ikiwemo:
🧚🏻‍♂️Kuondoa mba kichwani
🧚🏻‍♂️Kuondoa miwasho
🧚🏻‍♂️Kuponya vidonda, mapunye na magonjwa yote ya ngozi kichwani
🧚🏻‍♂️Yanakuza nywele kwa haraka 
🧚🏻‍♂️Huzuia nywele kukatika na kuzipa nywele unyevu unyevu.

SOMA ZAIDI HAPAπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌ
https://hairandskinlovers.blogspot.com/2019/09/22-fahamu-zaidi-kuhusu-mafuta-ya.html?m=1

INAENDELEA❤️

51. MAFUTA MAZURI YA NYWELE AINA ZOTE

Tulishaangalia aina mbili za mafuta mazuri ya nywele aina zote, leo tumalizie aina ya tatu ili kila mmoja aweze kuchagua mafuta yake anayotaka ayatumie na yatakayomletea matokeo chanya.

AINA YA TATU: MAFUTA YA NAZI (COCONUT OIL)


Haya ni mafuta ambayo yanajulikana sana na watu wengi kuipelekea kupewa jina la “Mafuta mama”. Mafuta haya yapo ya aina nyingi sana kutegemea na njia anayotumia mtu kuyatengeneza, pia yapo fake na original (kuwa makini wakati wa kuchagua). Siku zote tumia ambayo yameandikwa “VIRGIN COCONUT OIL” au “MAFUTA MWALI” haya ndio huwa pure means hayajachakachukiwa.
Mafuta ya nazi yana matumizi mbalimbali tofauti na urembo wa ngozi na nywele. Umaridadi wake unatokana na uwepo wa asidi mafuta muhimu sana ya “Lauric” ambayo ina uwezo wa kupambana na bacteria, fangasi, sumu, vijidudu nyemelezi na maambukizi. Mafuta haya yanatumika kupikia pia.

Faida  za mafuta ya nazi  (urembo)
🧚🏻‍♂️Hukuza na kurefusha nywele kwa muda mfupi
🧚🏻‍♂️Huondoa mba na kulainisha nywele
🧚🏻‍♂️Hutibu matatizo yote ya magonjwa ya ngozi kichwani
🧚🏻‍♂️Hulainisha ngozi
🧚🏻‍♂️Husaidia kuzipa nywele unyevu unyevu

Faida za mafuta ya nazi (mengineyo)
🧚🏻‍♂️Huzuia na kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu
🧚🏻‍♂️Huzuia uwezekana wa kupata kansa
🧚🏻‍♂️Yanaongeza kinga ya mwili maradufu
🧚🏻‍♂️Yanaongeza nguvu ya ubongo
🧚🏻‍♂️Dawa nzuri ya kutibu matatizo ya mifupa
🧚🏻‍♂️Husaidia kushusha uzito (kupunguza uzito)
🧚🏻‍♂️Husaidia kuondoa msongo wa mawazo (stress)
🧚🏻‍♂️Huimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
🧚🏻‍♂️Hutibu matatizo ya kongosho na kibofu cha mkojo
🧚🏻‍♂️Yanatibu na kuimarisha mfumo wa misuli ya mwili
🧚🏻‍♂️Huzuia meno kuoza na maradhi ya fizi
🧚🏻‍♂️Huongeza ufanisi wa ini na figo
🧚🏻‍♂️Yanaondoa mawe kwenye figo na kibofu cha mkojo
🧚🏻‍♂️Yanaondoa baridi yabisi
🧚🏻‍♂️Yanatibu kisukari aina ya kwanza
🧚🏻‍♂️Yanatibu maambukizi ya fangasi
🧚🏻‍♂️Husaidia kazi ya tezi koromeo (Thyroid glands)
🧚🏻‍♂️Yanaweka sawa hormone
🧚🏻‍♂️Huzuia kuonekana mzee wakati umri bado (anti aging)

MAISHA YA CHUO KIKUU NA MAPENZI

1st year

nikiwa nimekaa leacture room nikimuangalia msichana aliyekaribu yangu,niliyekuwa nikimuita "Bestfriend"nilikuwa nikimuangalia nywele zake nzuri na sura yake ya upole huku nikitamani awe wangu,lakini yeye hakuwa akitamani hilo na nilikuwa nikilitambua hilo.
Baada ya leacture,alikuja kwangu na kuniomba notes za siku ya nyuma kwa sababu hakuweza kuingia darasani hiyo siku iliyopita.baada ya kumpa akasema "asante" na kushikana mikono na mimi.I wanted to tell her,i want her to know that i don't want us to be just friends,i love her but i'm just to shy,and i don't know why


2nd year

Simu yangu iliita,kupokea alikuwa yeye alikuwa akilia akinielezea jinsi gani boyfriend wake broke her heart,she asked me to come over because she didn't want to be alone,kwa kuwa ni rafiki yangu kipenzi ilinibidi kwenda kumfariji,as i sat next to her on the sofa,nilikuwa nikimuangalia Machoni nikitamani awe wangu.Baada ya masaa mawili baada ya kuangalia nae movie mbili tatu na kula nae chakula pamoja akarudi katika hali yake ya kawaida,hivyo akaamua kwenda kulala,before akaniangalia na kuniambia "asante" na kunipa tabasamu tamu,i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.

3rd year

Siku moja kabla ya Tamasha la muziki chuoni alikuja kwenye meza yangu leacture room na kuniambia "Boyfriend wangu amepata udhuru hivyo naomba unipe campan katika tamasha la muziki leo usiku" kwa kuwa tuliwekeana promice kwamba ikitokea kila mmoja wetu amekosa mtu wa ku-date nae basi tutaenda pamoja just as "bestfriends".hivyo tukaenda.
katika tamasha baada ya kila kitu kuisha na muziki kufungwa,nilikuwa nimekaa nje ya ukumbi nikimuangalia jinsi alivyokuwa akicheka na rafiki zake,she saw me looking to her she smiled at me,i want her to be mine lakini yeye alikuwa hafikirii hilo kabisa na nilikuwa nikilitambua hilo,then she said to me "nimekuwa na muda mzuri na wewe asante sana" and she gave me a sweet smile.I want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.

Graduation Day

siku,wiki kisha mwezi ukapita ilikuwa ni mahafali yetu tukimaliza masomo ya chuo,akiinuka kwenda kutunukiwa shahada yake ya uchumi nilikuwa nikimuangalia akiwa amependeza sana siku ile,i wanted her to be mine,but she didn't notice me like that,and i knew it.
kabla watu hawajatawanyika kwenda makwao,alikuja kwangu akiwa na vazi lake la mahafali,na kulia pale nilipomkumbatia akainua kichwa chake na kuniambia "you are my bestfriend asante sana" i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.

Miaka michache baadae

Nikiwa kanisani Yule Msichana akiwa anaolewa sasa,nilimuangalia akisema "ndiyo nakubali " and drive off to new life,kaolewa na mwanaume mwingine,i wanted her to be mine,but she didn't see me like that,and i knew it.
but before she drove away,alikuja kwangu na kusema "asante sana" and kissed me on the cheek.I want to tell her to know that i dont us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.

Kwenye Mazishi

Miaka ilipita i looked down katika jeneza lilokuwa na msichna ambaye alikuwa ni "bestfriend" wangu,Katika Service ya mazishi wakasoma diary ya Bestfriend ambayo alikuwa akiiandika enzi za maisha ya chuo'

Diary yake ilikuwa Ilikuwa ikisomeka hivi
I stare at him napenda awe wangu,but he doesn't notice me like that,and i know it,i want to tell him,i want him to know that i dont want us to be just friends,i love him but i'm just to shy,and i dont know why.I wish he would tell me he loved me!

Nilipiga magoti huku nikilia nikijisemea moyoni i wish ningemwambia tu ukweli,nimeshachelewa sipo nae tena katangulia mbele za haki i cried!!

Vunja ukimya

Wednesday, December 11, 2019

49. JINSI YA KUKUZA NYWELE KWA HARAKA ZAIDI

Leo tuangalie treatment au steaming unayoweza kuifanya mara kwa mara ili upate nywele ndefu na zenye afya baada ya muda mfupi sana (Baada ya mwezi unaanza kuona mabadiliko). Hii treatment inatumika kwa watu wenye nywele za aina yoyote.

Mahitaji
🧚🏻‍♂️Yai moja la kienyeji
🧚🏻‍♂️Hinna ya unga

JINSI YA KUANDAA
🧚🏻‍♂️Tengeneza mchanganyiko wa yai (lote) na hinna kiasi ili upate mchanganyiko mzito kidogo (paste).
🧚🏻‍♂️Paka katika mizizi ya nywele
🧚🏻‍♂️Ukimaliza kupaka vaa shower cap
🧚🏻‍♂️Unaweza funga na lemba juu ya shower cap ili zipate joto zaidi
🧚🏻‍♂️Kaa navyo kwa muda wa masaa mawili
🧚🏻‍♂️Baada ya hapo osha kwa maji ya kawaidia na shampoo
NB: Tumia maji mengi ili kuondoa harufu ya mayai, pia yawe ya baridi (yasiwe ya moto wala vuguvugu-utapata harufu ya mayai ya kuchemsha)
🧚🏻‍♂️Kausha nywele zako kwa tshirt au kitambaa cha cotton
🧚🏻‍♂️Fanya hii kila wiki utapata matokeo ya haraka zaidi

Mambo ya kuzingatia
🧚🏻‍♂️Nywele hazichanwi zikiwa na maji (zikiwa mbichi); Hii husababisha kung'oka kwa nywele na kusababisha upungufu wa nywele (nywele kuwa chache).
🧚🏻‍♂️Nywele zikishakauka, paka  mafuta ya nazi, au your favourate muhimu upake katika mizizi ya kichwa na upende zaidi kutumia mafuta ya kimiminika au ya maji
🧚🏻‍♂️Wakati unapaka mafuta kichwani kichwa kiinamishe chini, kiangalie chini ndio upake mafuta kichwa chako husaidia msukumo wa damu kufikia katika kichwa vizuri, kupata stimulation tumia ncha za vidole kufanya massage kichwani taratibu kwa mda wa dakika tano, ukimaliza anza kuzichana taratibuu mpaka zilainike na uzibane.
🧚🏻‍♂️Jaribu kwa siku uchane nywele mara mbili asubuhi na jioni (kama hujasuka), na nywele muda wote ziwe zenye mafuta. 
🧚🏻‍♂️Jizoeshe m kufanyia massage kichwa chako kila wakati unaopaka mafuta kichwani.

KUMBUKA: Uhai wa nywele ni mafuta na maji kama  ilivyo uhai wa binadamu utakuepo iwapo kuna maji na chakula

Tuesday, December 10, 2019

48. MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WALE WANAOWEKA DAWA NYWELE

HAYA NI MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
kuchagua uweke dawa gani ya box au ya kopo hutegemea na ngozi yako ya kichwa kama iko sensitive yaani inaungua haraka unashauriwa dawa ya box,na wenye ngozi ambayo sio sensitive yaani haiungui haraka mnashauriwa kuweka dawa ya kopo au yoyote utakayoipenda wewe.

Dawa zimegawanyika makundi matatu
🧚🏻‍♂️Regular/normal
🧚🏻‍♂️Super/extra
🧚🏻‍♂️Mild
Hii mild siku hizi haipo na  hapa tutazungumzia dawa mbili tu regural ambayo jina lingine ni normal na super ambayo jina lingine ni extra .
Unashauriwa kuangalia kopo au box lako kujua unatumia dawa gani sio kujiwekea tu ilimradi hlf unataka kuwa na nywele nzuri.

MATUMIZI
🧚🏻‍♂️Normal /regular hii ni dawa ambayo unashauriwa utumie  mtu mwenye fine na medium hair yaani mtu mwenye nywele laini na zisizo ngumu wala laini zipo kati

🧚🏻‍♂️Extra hii inatumika for course hair,yaani nywele ngumu
NB: Ijue  nywele yako ni ya aina gani usijipakie dawa tu, kuna watu wanalalamika nywele haishiki dawa ni ngumu kumbe anapaka dawa ya watu wenye nywele laini normal badala ya kupaka extra,na mwenye nywele laini anapaka super za watu wenye nywele ngumu utaishia kulia nywele nyepesi zinanyonyoka kumbe tatizo ni lako.

MAMBO YA KUZUNGATIA
🧚🏻‍♂️Zingatiab muda wa kukaa na dawa kichwani; Usizidishe wala kupunguza bali  fuata maelekezo ya muda wa kukaa nayo huwa wanaanddika kwenye box na kopo.

🧚🏻‍♂️Muda  wa kuretouch inafuatana na jinsi nywele zilivyoota muda wa chini wa kufanya retouch ni wiki 10-12 na kuendelea usiwahi chini ya hapo kwani zilizootea zitakuwa chache ukizidi weka dawa nywele ambayo haijaotea hukatika

🧚🏻‍♂️Paka  dawa nywele iliyoota tu usiguse yenye dawa,upake chini tu.

🧚🏻‍♂️Ukimaliza  kuweka dawa jitahidi kufanya steaming(deep conditioner)

🧚🏻‍♂️Kuwa  na mazoea ya kusoma,product kilichoandikwa usikurupuke.

🧚🏻‍♂️Zipende  nywele zako na  zielewe zinataka nini.

Ukifuata mambo hayo utazipenda nywele zako tofauti na wengine wanavozichukia nywele zao za dawa.

Monday, December 9, 2019

47. NJIA 10 ZA KUFANYA NYWELE ZIWE ZA KUVUTIA NA ZENYE AFYA

kuna vitu vingi vinavyoweza kufanya nywele zako zikakosa afya na mvuto, vitu kama vumbi, upepo, mvua, jua, maji na madawa yanayowekwa  kwenye nywele zetu pamoja na vyakula tunavyokula ni chanzo kikuu cha nywele zetu kuharibika,  kukosa afya pamoja na  mvuto. leo nimekuletea vidokezo vichache vya jinsi ya kutunza nywele zako kiusahihi zaidi.
🧚🏻‍♂️Kata ncha za nywele zako
kukata ncha za nywele zako kunasaidia kufanya nywele zako kujizaa upya, mara nyingi seli katika ncha za nywele hufa. Seli zinapokufa huzuia  nywele zinazozaliwa  kustawi vyema na hivyo kuzifanya nywele zako kukosa afya. Japo wanawake wengi huwa hawapendi kukata ncha za nywele zao wakihofia nywele zao kuonekana fupi lakini  ukweli ni kwamba unapokata ncha za nywele zako unasaidia nywele zako kupata nafasi ya kukua vizuri na kuwa zenye afya nzuri na kuvutia.

🧚🏻‍♂️Osha  nywele zako angalau mara moja kwa wiki
Kuosha  nywele zako angalau mara moja kwa wiki kutasaidia kuzifanya nywele zako ziwe na afya na safi; hata  kama uko busy sana basi jitahidi isipite wiki mbili bila kuziosha  nywele zako.

🧚🏻‍♂️Tumia  shampoo inayoendana na nywele zako
Tumia  shampoo inayoendana na nywele zako, kuna nywele za aina tofauti. kuna nywele kavu, zenye mafuta, mchanganyiko, na pia kuna nywele nyepesi, laini, ngumu, nzito nk.. Zipo  aina tofauti za shampoo zinazoendana na aina ya nywele zilizopo, hivyo  basi ni vyema unapotaka kuosha nywele ukajua ni aina gani ya shampoo utumie, pia kwenye condition napo unatakiwa kufanya hivyo hivyo.

🧚🏻‍♂️Zipe  nywele zako nafasi
Nywele  nazo huitaji nafasi,kuchana nywele kila siku,  kuzipaka nywele jelly kila siku, kuzichana mitindo tofauti, kuziwekea gundi na mafuta tofauti tofauti huzifanya nywele zako zichoke na kukosa afya, hivyo  unatakiwa mara moja moja unazipa nywele zako nafasi ya kupumzika na kupumua  kwa kusuka mtindo ya kawaida au rasta za mabutu. ​

🧚🏻‍♂️Usichane  nywele kwa nguvu zikiwa mbichi.
Jaribu  kuzichana nywele kwa chanuo kubwa, au jaribu kuziacha mpaka zikauke ndo uzichane. unapochana nywele mbichi tumia kitana kikubwa na chana taratibu ukianzia nyuma kuja mbele. kuchan nywele zikiwa mbichi bila kufuata utaratibu kutafanya nywele zako zikatike na ziharibike.

🧚🏻‍♂️Zilinde  nywele zako unapokuwa unaogelea
Unapokua  unaogelea baharini au kwenye bwawa la kuogelea, jaribu kuzifunika nywele zako au zipake mafuta ya kuzuia  zisiharibike na maji, na unapotoka kuogelea zisafishe nywele zako kwa maji safi na uzikaushe.

🧚🏻‍♂️Kula  vyakula venye protein na matunda kwa wingi
kula vyakula venye protin na matunda kutasaidia kuimarisha  afya ya nywele zako na kuzifanya ziwe nzuri na za kuvutia.

🧚🏻‍♂️Zifunge  nywele zako kabla ya kulala
Unapotaka  kulala hakikisha unazifunga nywele zako, unaweza kuzisuka mabutu au kuzifunga  vizuri na kuzibana. Kulala huku  ukiwa umeziachia nywele zako hufanya nywele zikatike na kuharibika

🧚🏻‍♂️Tumia  mafuta asili
Badala  ya kutumia mafuta yenye kemikali nyingi kutoka viwandani, jaribu kutumia mafuta ya asili katika kutunza nywele zako. Tumia  mafuta kama ya mnyonyo au  nazi au parachichi kupaka nywele zako.

🧚🏻‍♂️Zilimde  nywele zako na jua
Wakati  utakapokuwa unaelekea kwenye sehemu yenye jua kali, vumbi au upepo. zilinde nywele zako kwa kuzifunika na kofia, scarf au mtandio. pia unaweza kuzipaka sunscreen.

Sunday, December 8, 2019

46. NJIA YA KUFANYA NYWELE ZISIWE KAVU,ZISIKAKAMAE,ZIWE LAINI

Hii ni moja ya vitu ambavyo watu wengi wanaotunza nywele zao wanateseka navyo na wengi bado hawajajua solution ni nini. Wengi wanalalamika kuwa na nywele kavu, kuuma wakti wanachana, kukatika nk. Sasa leo tuangalie vitu unavyotakiwa kufanya ili  nywele zisikakamae au kuwa kavu, zisiume wakati wa kuchana na kukatika.

VITU VYA KUFANYA
🧚‍♀️DEEP CONDITIONING (STEAMING)
Hii ni  solution ya kwanza , kufanya steaming nywele zako mara kwa mara inasaidia sana. Kila kampuni yenye products za Natural hair inakua  na shampoo/ conditioner /moisturizer / detangler nk kulingana na matumizi yako. Ni muhimu sana kuchagua products/bidhaa zenye ubora kulingana na nywele zako (usiangalie gharama ila angalia ubora).
Hivyo  basi kama wewe una nywele kavu. baada tu ya kuosha lazima upake conditioner ili kulainisha nywele zako at list mara moja kwa wiki au kila unapoisha nywele zako.

🧚‍♀️ KUVAA KOFIA YA SATINI/KUFUNGA KITAMBAA CHA SATINI/ KUTUMIA MTO WENYE FORONYA YA SATUNI ULALAPO
Hii inasaidia sana kutunza unyevu unyevu (kuwa moisturized) maana usipovaa usipofanya hivyo itakua ngumu  kutunza unyevu nyevu wa nywele. Najua inakera kulala umejibana kichwaa ila furaha huwa zaidi asubuhi utapoamka huku nywele zako zikiwa laini na sio kavu na pia inazuia usumbufu pamoja na kuchafua foronya nyingine na mafuta ya nywele. Hii pia  inapunguza  nafasi kubwa ya nywele kukatika.

🧚‍♀️KUBADILI  BRAND / PRODUCT UNAYOTUMIA
Yes ni kweli ulishauriwa na muuzaji au uliisoma online ina review nzuri au ulikutakana na mdada mwenye natural hair ambaye alikupa ushirikiano ulipomuuliza anatumia product gani ya nywele akakujibu nawe ukaenda nunua ukaanza itumia, lakini sio kila product inamfaa kila mtu kwa sababu ya utofauti wa aina ya nywele; Hivyo ukiwa umetumia hair product kwa muda na huoni matokeo ni muda wa kuachana nayo na kujaribu nyingine mpaka nywele zako zitakapokubali ndio utabaki na hiyo.

🧚‍♀️PUNGUZA  MIONZI YA KUZIPASI  AU KUNYOOSHA NYWELE (ACHA KUTUMIA MOTO)
Ni  kawaida sana siku  ukitaka kubadili muonekano au hair style ukaamua kuzichoma/kusipasi au kunyoosha nywele zako kwa kutumia moto (umeme). Unashauriwa  kupunguza temperature au kutumia kinga (mafuta maalum) ambayo inafanya nywele zako zisipate damage wakati ya kuzinyoosha hii itakusaidia kutunza moisture sambamba na kupunguza ukatikaji wa nywele zako.

🧚‍♀️MAJI NDANI NA NJE
Yes huwezi pinga hili maji ndio  kila kitu kwa afya ya mwili na hata maisha ya kila siku. Unatakiwa kunywa maji  meengi uwezavyo na pia unatakiwa kutumia products hasa Leave in Conditioner ambazo ni WATER BASED PRODUCTS. Na pia  maji ndo product isiyo ya bei ghali na iliyo rahisi kupatikana na  kuitumia. Hivyo kunywa maji mengi uwezavyo na kunyunyizia maji kwenye nywele zako.

Saturday, December 7, 2019

45. VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA UKIWA KWENYE TRANSITION PERIOD

Hizi ni tips/mambo muhimu mtu anavyotaikiwa  kufanya akiwa kwenye transition yaani kutoka nywele yenye dawa kwenda nywele natural bila kufanya big chop (bila kukata nywele zote).

🧚‍♀️Usiweke  dawa tena kuruhusu nywele ziotee
🧚‍♀️ Punguza matumizi ya moto au usitumie kabisa.
🧚‍♀️Zingatia sana kufanya pre poo
NB: Fanya  pre_poo kabla ya kuosha nywele kwa shampoo nzuri (isiyo na viambata sumu)
🧚‍♀️Usitumie  shampoo zenye viambata sumu kama vile sulphate kwa sababu ni kemikali ambayo si rafiki kwa nywele hasa natura;  unaponunua shampoo hakikisha unasoma ingredients kwa umakini na kuhakikisha ni sulphate free shampoo
🧚‍♀️Chana  nywele zako vizuri ikiwezekana tumia mikono kwanza wakati wa kuchambua kisha zichane maana vipilipili vyetu (nywele nyingi za kiafrica) zina  tabia ya kujifunga sana
🧚‍♀️Fanya  steaming (deep conditioner) mara kwa mara na ikiwezekana hata kila wiki.
🧚‍♀️Tumia  satin cap wakati wa kulala; unaweza kvaa kofia ya satini au mto wako uvishe foronya ya satini.
🧚‍♀️Suka  misuko kinga ili kulinda nywele zako kila wakati na hufanya nywele kukua, na kuzuia kukatia /misuko kinga yaani PROTECTIVE  style
🧚‍♀️Zipe  nywele zako unyevu; Maji maji  ni rafiki wa nywele hasa nywele natural,ndio maana unatakiwa uwe na spray bottle (kinyunyuzi) kiungo kikubwa katika kuzipa nywele unyevu ni maji huwezi kuwa naturista kama huna spray bottle.
🧚‍♀️Trim  nywele zako yaani ondoa  nywele zisizo na afya na zenye dawa,mpaka utakapobaki na nywele natural tu. Pia kwa wenye natural hair   trim zile nywele za  juu zisizo na afya mara kwa mara
🧚‍♀️Usitumie taulo kufuta nywele zako bali tumia  t-shirt hasa ya cotton kufuta nywele zako.
NB: Ni lazima uwe na tshirt maana t-shirt  inabaki na nywele na pia huvuta  nywele kitu ambacho kinachangia sana katika  kukatika kwa nywele.
🧚‍♀️Chana nywele  zako kwa mafungu pindi unapoosha
NB: kufanya hivyo kunasaidia nywele zako kutakata maana unaosha kidogo kidogo tofauti ukiosha kwa jumla unakata mafungu manne au zaidi kulingana na uwingi wa nywele zako.

Friday, December 6, 2019

44. VITU VYA MUHIMU VYA KUZINGATIA UNAPOTAKA, KUSUKA MSUKO KINGA (PROTECTIVE STYLE)

VITU VYA MUHIMU VYA KUZINGATIA UNAPOTAKA, KUSUKA MSUKO KINGA (PROTECTIVE STYLE)
Protective style kwa kiswahili ni Msuko kinga, huu unasukwa ili kuzikinga nywele za asali au za dawa kukatika, kuharibika na hivyo kuzifanya zikue vizuri na zisiwe nausumbufu wowote.

🧚‍♀️Msuko kinga au protective style ni  msuko ambao unaweza kukaa kichwani kwako kuanzia siku tano na kuendelea, mpaka mwezi inatokana na aina ya nywele.

Msuko kinga (Protective style) unaweza kuwa;
πŸƒ Nywele za rasta (box braids)
πŸƒNywele za  mkono (flat twist)
πŸƒNywele  za uzi (african threads) nk.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUSUKA
🧚‍♀️Osha nywele zako kwa shampoo;  Unashauriwa utumie sulfate free shampoo.
(Kwa nini utumie  sulfate free shampoo nilifundisha, post zilizopita pitia)
🧚‍♀️Fanya deep conditioner (steaming)
Hii huzuia nywele  kukatika, inakuza nywele na kufanya nywele ziwe na afya; Utakaa na steaming ndani ya nusu saa au dakika 30.
🧚‍♀️Detangle nywele zako ipasavyo
🧚‍♀️Chana  nywele zako kuanzia  juu kushuka chini,wengi tumezoea kuchana kuaanzia chini kupanda juu lakini hii ina madhara mengi kama vile:
-Inasababisha nywele kukatika
-Nywele utaona hazikui
🧚‍♀️Unachana nywele kimafungu kama ni ndefu na nyingi; yaani zilizojaa
🧚‍♀️Hakikisha  unatumia chanuo lenye meno mapana.
🧚‍♀️Moisturize (zipe nywele zako unyevu.
Kwa nini  tunazipa unyevu kwa sababu nywele kavu ni rahisi kukatika,huwa ngumu na kuuma pia.
🧚‍♀️Baada ya hapo suka  msuko wako.

43. FAHAMU ZAIDI KUHUSU BIG CHOP (KUKATA NYWELE ZOTE)

Big chop ni nini?

Big chop ni kitendo cha kukata nywele kabisa na kuanza safari mpya ya nywele za asili.
Watu wengi hufanya big chop kutokana na kuharibika kwa nywele zao na kupoteza mvuto halisi wa nywele.

Baadhi ya  sababu zinazopelekea nywele kuharibika ni:
🧚‍♀️Matumizi ya kemikali yakizidi katika nywele; nywele inakosa  afya na mvuto.
🧚‍♀️Matumizi makubwa ya moto wa aina yoyote ile kwenye nywele.
KUMBUKA: Moto ni adui mkubwa wa nywele  za dawa na zisizo na dawa (natural) na nywele za dawa (relaxed)
🧚‍♀️ Nywele kukosa afya na kuwa nyepesi kwa sababu ya kuzistress nywele, kutodetangle ipasavyo au kuchana nywele kila wakati.
Ukiona dalili kuwa nywele zako hazina afya nzuri   unashauriwa kufanya bigchop na kuanza upya kabisa.

NB: Unashauriwa  kutumia products  zinazoemdana na nywele yako

Thursday, December 5, 2019

42. JINSI YA KUACHA KUTUMIA DAWA NA KUWA ASILI (NATURAL)

Hili ni swali ambalo watu wengi wenye nywele zenye dawa wamekua wakiuliza; Je nifanye nini ili nywele zangu ziwe za asili?. Leo tuangalie njia kuu mbili ambaxo unaweza kutumia ili kurudi kuwa natural (kuacha kabisa kutumia dawa ya nywele). Pia tutaangalia na hasara na hasara ya kila njia maana faida yake  zote in general ni kupata  nywele natural.

NJIA YA KWANZA
1.TRANSITION METHOD
Hiki ni kitendo cha kuacha dawa / matumizi ya dawa za nywele na kuruhusu ikue yenyewe huku ukikata (au kutrim) kidogo kidogo nywele za juu mpaka  utakapimaliza nywele zote zenye  dawa.

FAIDA YA TRANSITION 
🧚‍♀️Unapata  muda wa kuisoma nywele yako vizuri
🧚‍♀️Kama haupo huru na nywele fupi unabaki na nywele zako ndefu
🧚‍♀️Hausubiri kukua kwa nywele
🧚‍♀️Wakati wa transition unamuda wa kustyle na kusuka nywele zako upendavyo

 HASARA ZA TRANSITION
🧚‍♀️Texture ya nywele inakua tofauti
🧚‍♀️Process  ya transition inachukua muda mrefu kuliko kuzikata kabisa
🧚‍♀️ Nywele kukatika ni lazima na huwezi kueluka;  Kwani nywele yenye dawa zina heat  na chemical   damage hivyo ni lazima zitoke tu.

VITU VYA KUZINGATIA KIPINDI HIKI
🧚‍♀️Katika kipindi hiki ni lazima KUEPUKA  na wala KUJARIBU kutumia moto hotcombs na blow dryers vile vile usipige  pasi nywele zako utaharibu za chini zinazopelekwa kuwa natural.
🧚‍♀️Acha kabisa  kutumia bidhaa zenye viambata sumu especially SULFATES  NA PARABENS 🧚‍♀️PROTECTIVE style; Fanya protective style kupunguza manyanyaso ya kila siku kwako personally (maumivu ya kuchana nywele na kuzitreat) pia kwa nywele kusumbuliwa sumbuliwa kila siku. Protective style ni mitindo ambayo unaweza kufanya na kukaa nayo atleast siku 5 au zaid bila kuchana.
🧚‍♀️ kumoisturize (kuzipa unyevu)  nywele zako
🧚‍♀️ TRIM ncha mbovu mara kwa mara vizuri zaidi ni   baada ya miezi 2 au zaid ili kuondoa split ends (ncha zilizochoka) - Unatumia mkasi ila sio wa nguo.

NB: Pale nywele za asili zinaporefuka na kukutana na za dawa  ndipo kazi itaanza maana  Hii sehemu huwa ni  dhaifu sana Jitahid kufanya deep conditioner (steaming kwa lugha iliyozoeleka) kila  wiki ili kulinda na kuzipa nguvu nywele.

NJIA YA PILI
2. BIG CHOP (BC)
 Hii ni kwa wale wanaotaka kuwa na nywele  natural kuanzia mwanzo sasa wanakata nywele zote za dawa na kubaki na nywele  vifupi - TWA (teeny weeny Afro). In general in KUNYOA tu.

 FAIDA ZA BIG CHOP
🧚‍♀️Hausubiri  muda mrefu kuanza kuzitunza nywele zako kiusahihi
🧚‍♀️Unaanza fresh kabisa  bila dawa
🧚‍♀️Unakua na uwezo wa kujua aina ya nywele zako haraka na hivyo itakua rahisi kuzihudumia.

HASARA ZA BIG CHOP
🧚‍♀️Unasubiri kidogo ili  nywele zikue
🧚‍♀️Unatakiwa  uitambue nywele yako haraka
🧚‍♀️Inaanza  na style mpya ya kuwa na nywele fupi.

BUT: Yote ni maamuzi yako  angalia ipi itakua njia sahihi kwako.
La muhimu zakdi ni  KUEPUKA  MATUMIZ YA MOTO WA AINA YOYOTE ILE KWENYE NYWELE.

Tuesday, December 3, 2019

41. NJIA YA KUKUZA NA KUREFUSHA NYWELE ZAIDI

Najua watu wengi wanapenda kua na nywele nzuri, ndefu na za kuvutia. Waafrika  nywele zetu sio kama za wazungu so zinahitaji matunzo na uangalizi sana ili zirefuke na kuwa nzuri zaidi. Kuna steaming (treatments)  nyingine zinaleta matokeo haraka na nyingine taratibu . Leo tujifunze steaming ya asili yenye matokeo yanayoonekana ya haraka zaidi.

MAHITAJI
🧚‍♀️Ndizi mbivu 1
🧚‍♀️Yai la kienyeji 1
🧚‍♀️Asali(mbichi)-vijiko 5 vya chakula
🧚‍♀️Grand malt-vijiko 10 vya chakula

JINSI YA KUANDAA
🧚‍♀️Safisha ndizi na kumenya vizuri
🧚‍♀️Changanya vitu hivyo vyote kwenye na usage kwenye blender  ili upate uji wake safi.
🧚‍♀️Osha nywele zako kwa shampoo isiyo na viambata sumu
🧚‍♀️Kausha nywele zako kidogo kuondoa maji yanayochuruzika
🧚‍♀️Paka  mchanganyiko huo kichwani
🧚‍♀️ Vaa shower cap nywele iive vizuri.
🧚‍♀️Kaa na shower cap kwa muda wa lisaa limoja.
🧚‍♀️ Osha  nywele zako vizuri kwa kutumia maji tu, bila shampoo
🧚‍♀️Fanya  hivi kila baada ya wiki mbili na baada ya mwezi mmoja utagundua kuwa nyweke zako zimerefuka.

NB: kuna watu watajiuliza yai ni protein iweje unaweka baada ya wiki mbili? Yes ni PROTEIN lakini uwepo wa grand malt (ingredients zake) na asali zinaleta mchanganyiko ambao hata ukitumiwa kila wiki bado hautaleta madhara ya protein nyingi kwenye nywele❤️.

40. JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA NAZI (2)


NJIA YA  PILI
🧚‍♀️Chukua nazi iliyokomaa vizuri (sio zile  changa)
🧚‍♀️Kuna  nazi vizuri  kwa kutumia njia yeyote iliyo rahisi kwako  kama una mbuzi,
food processor, blender, grater au grapefruit spoon yoyote unaweza kutumia.
🧚‍♀️Chukua  maji ya vuguvugu kiasi kisha ongeza kwenye ile nazi uliyokuna
🧚‍♀️ Changanya na mikono yako kwa dakika 1 hadi 2
🧚‍♀️Kamua vizuri kwa kutumia chujio la nazi au cheese cloth ili upate tui la nazi.
🧚‍♀️Unaweza kurudia mara kadhaa kuweka maji ya vuguvugu ili kutoa matui yenye mafuta yote (mafuta yote kwenye nazi in general).
🧚‍♀️Ukishapata  tui  weka katika chupa na liache likae kwa  masaa 24 ili mafuta yajitenge na maji.
 πŸ§š‍♀️Au unaweza weka jikoni (medium heat) kwa muda wa saa moja au mpaka maji yameondoka na yaliyobakia ni mafuta tu (au kwa kiwango kikubwa)
🧚‍♀️ Toa mapovu ya juu halafu weka mafuta yako katika chupa utakayoandaa.
🧚‍♀️Hadi hapo mafuta yako yapo tayari kutumia.

ITAENDELEA NJIA YA TATU❤️

Sunday, December 1, 2019

39. UTAJUAJE KAMA NYWELE ZAKO ZINA AFYA (HEALTHY HAIR)

Unaweza kuwa na nywele ambazo unaweza kukaa nazo lakini hujui kama ni nywele zenye afya au lah; Jaribu kuzichunguza vizuri nywele zako na kama zina sifa zifuatazo basi ni nywele zenye afya

🧚🏻‍♂️Hazikatiki kabisa au zinakatika kidogo sana

🧚🏻‍♂️Zinang’aa naturally
Hapa nywele zinakua zinang’aa vizuri na kuvutia hata bila kutumia sprays.

🧚🏻‍♂️Zinakaa na kupokea unyevu kirahisi

🧚🏻‍♂️Zinakua laini na haziuki wakati wa kuchana
Hapa hata kwenye kudetangle inakua ni rahisi sana unaona kabisa vidole vinapita kirahisi zaidi na hata ukizipa  unyevu inakua ni rahisi sana kuzichana

🧚🏻‍♂️Zinakua na nguvu (sio nyepesi sana) na kuwa nzito
Hapa nywele zinakua na nguvu na hata pale unapochana unaona kabisa kukatika ni ngumu sana labda utumie nguvu zaidi au ukosee uchanaji wake.

🧚🏻‍♂️Uwezo wa kuvutika kirahisi
Hapa hata kama nywele zako zimeshrink (ambayo ninsifa pia ya nywele zenye afya) lakini zinakua na uwezo wa kuvutika maana yake nywele sio ngumu ila ni nzito.

38. KWA NINI NYWELE ZAKO HAZIKUI

Hili ni swali ambalo watu wengi wamekua wanauliza, mbona nywele zangu hazikui, imekua miaka kadhaa toka nianze kufuga nywele lakini ziko pale pale, haziongezeki wala kukua. Nataka tu nikukumbushe leo nywele hazijawahi kuacha kukua na wala hazitaacha kukua, zitaendelea kukua mpaka siku unayofariki (kuondoka duniani). Kama nywele zako zimekua na ujazo na kimo hivho hicho kwa muda mrefu jua kua nywele zako hazijaacha kukua ila zinakatika (kiwango kinachokua ni sawa na kinachokatika au kinachotoka/so work done=zero). Kwa hiyo swali unalotakiwa kujiuliza ni kwa nini nywele zako zinakatika?.
Hizi ni baadhi ya sababu kwa nywele kukatika

🧚🏻‍♂️Namna ya kustyle na kubana nywele kwa kutumia gels mbalimbali na kukaa nazo muda mrefu
🧚🏻‍♂️Detangling isiyo sahihi (kutumia nguvu na kufanya haraka haraka)
🧚🏻‍♂️Viambata sumu (harmful chemicals)
🧚🏻‍♂️Misuko hatarishi inayokaza sana nywele
🧚🏻‍♂️Overstyling (kubana sana nywele kwa muda mrefu)
🧚🏻‍♂️Kukosa umakini na nywele zako
🧚🏻‍♂️Kutotumia vifaa sahihi
🧚🏻‍♂️Kukosa unyevu na kutreat nywele zako zikiwa kavu
🧚🏻‍♂️Njia za kutunza nywele zisizo sahihi
🧚🏻‍♂️Kudetangle nywele kavu
🧚🏻‍♂️Kutokukata ncha
🧚🏻‍♂️Kutopata mlo kamili na kutokunywa maji ya kutosha
🧚🏻‍♂️Kuzipa nywele zako protein nyingi (Too much protein treatment)
🧚🏻‍♂️Kukosa kabisa protein

MOST IMPORTANT: Zipende nywele zako nazo zitakupenda na hayo yoteπŸ‘†πŸΏπŸ‘†πŸΏ unaweza kuyafanya endapo tu utazipenda nywele zako