Friday, July 10, 2020

89. KWA NINI UKATE NCHA ZA NYWELE


Katika kushauriwa ukuzaji wa nywele nzuri na zenye afya mara nyingi tunakuta tunaambiwa tukate ncha za nywele, lakini kukata ncha hizi za nywele kunasaidia vipi kukuza nywele? na je ni mara ngapi unatakiwa kukata hizi ncha?
TUJIFUNZE KIDOGO.....
Ncha za nywele ni zile nywele zilizopo mwishoni kabisa hizi huwa nyepesi kuliko nywele zote ni kama zimesha kufa, wengi hujiuliza kwanini nywele hizi ni nyepesi?
๐Ÿ‘‰๐Ÿป Ni kutokana  na matumizi ya moto na kuchana nywele vibaya, hivyo ili kukuza nywele zako kuwa ndefu na zenye afya ni vyema ukakata ncha. Ni kama katika kukata miti au michongoma ile ya juu hukua nakuwa mibaya wakati huku chini inashamiri kwa kupata matunzo mazuri lakini kama utaiacha ile ya juu basi itaharibu show nzima ya hii ya chini.
๐Ÿ‘‰๐ŸปNcha za nywele mara nyingi huwa zimechoka na hata rangi yake kubadilika, mara nyingi ncha huwa lighter kuliko nywele za chini, zina haribu muonekano mzuri wa nywele
๐Ÿ‘‰๐Ÿป Hata ukitumia pesa kiasi gani katika salon kama ncha za nywele zako hujakata zitaonekana lifeless hazitopendeza hata kidogo lakini pia husababisha ukatikaji wa nywele.
๐Ÿ‘‰๐ŸปPia huwezi kutibu Ncha kwa kufanya hair treatments, unachotakiwa kufanya ni kuzikata tu, utapoteza muda na fedha zako bure, split ends hazina tiba

JINSI YA KUEPUKA NCHA ZA NYWELE AU NYWELE KIUJUMLA
๐Ÿ‘‰๐ŸปKata ncha
๐Ÿ‘‰๐ŸปPaka mafuta nywele zako kabla ya kuziosha
๐Ÿ‘‰๐ŸปChana  nywele zako taratibu
๐Ÿ‘‰๐ŸปTumia chanuo lenye meno makubwa kuchana nywele
๐Ÿ‘‰๐ŸปPunguza matumizi ya moto katika nywele
๐Ÿ‘‰๐ŸปKula chakula bora na kunywa maji ya kutosha

Tuesday, July 7, 2020

88. JINSI YA KUKUZA NYWELE HARAKA

Kama  wewe umeanza kukuza nywele na nywele zako hazikui haraka kama ulivyotegemea basi inawezekana hauzitunzi vizuri.
Nitakuelezea njia unazoweza kutumia kukuza nywele zako haraka na kukujulisha ni makosa gani ambayo yamkini umekuwa ukiyafanya yanayositisha ukuaji wa nywele zako.
Kosa la kwanza: Watu  wengi wananyoosha nywele zao mara kwa mara. Mtu akifanya hivi, ndiyo basi tena anakuwa anaziua nywele zake na zitaanza kukatika wakati wa kuchana au muda wowote. Basi inabidi upunguze kutumia vifaa kama hivi ili nywele zako zikue.
Kosa la pili: Tunavyozinyoosha  nywele na kusuka mtindo wa rasta, nywele za kawaida au kushonea ‘weave’ zinakubalika, ila ukizichana na kuzibana nywele basi hapo kuna uwezekano mkubwa kwamba zitaharibika au zitakatika.
Kosa la tatu:  Kutokukata ncha  baada ya muda, ncha zinaweza kuanza kuchanika na inabidi uzikate ili nywele zikue vizuri kwa sababu ncha huchangia kwenye kusitisha ukuaji wa nywele na kukata nywele zenyewe. Unaweza kukata ncha sentimita mbili baada ya miezi mitatu au minne.
JINSI YA KUZITUNZA NYWELE
-Inatakiwa  uzisuke nywele zako mara kwa mara ili zisiharibike au zisikatike. Hivi utaweza hata kuzuia ncha zilizoharibika.
-Kama hujisikii kusuka nywele au kushonea ‘weave’ basi unaweza kuzibana kwa juu au kuzifunga ukitumia kitambaa bora tu kiwe cha silk ili nywele zako zisiharibike (unaweza kukitumia hata wakati wa kulala).
-Inabidi  upake mafuta kwenye kichwa chako mara kwa mara; hasa unapojisikia kama kichwa kimekauka au kama kinawasha. Mafuta mazuri kutumia kwa ajili ya ukuaji wa nywele ni mafuta ya nazi, castor oil, Moroccan, Jamaican au lavender. Unaweza pia kutumia mafuta mengine yoyote bora tu yasiwe ya mgando.
-Usizioshe  nywele kwa kutumia shampoo mara kwa mara kwa sababu inaondoa mafuta kwenye kichwa na nywele zako.
-Inabidi  uoshe nywele na conditioner kama unaona nywele zako sio chafu sana, ila kama unaona nywele zako ni chafu, basi osha ukitumia shampoo.
-Itakuwa  bora ukipaka mafuta kabla hujaosha nywele na uoshe nywele zako kila baada ya wiki moja na kama zinakatika, basi osha baada ya wiki mbili au tatu.
Vilevile ni muhimu kula vyakula vingi vyenye protini kama kuku, maharagwe au nyama yoyote inayokubalika.

Wednesday, July 1, 2020

87. JINSI YA KUFANYA HOT OIL TREATMENT


Hot oil treatment ni kitendo cha kupaka mafuta ya moto au yenye joto kichwanai (hasa kwenye ngozi ya kichwa).
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Hii inafanyika kwa kupasha mafuta joto kisha  hutumika kumassage kichwa chako ususani kwenye ngozi sio nywele, hot oil treatment ni muhimu kwa ngozi kavu(nazungumzia ya kichwa) kama ngozi yako ina kiwango kizuri cha maji au yamezidi usitumie hii itumike kwa wale wenye ngozi kavu tu ili kushtua ngozi kupokea virutubisho kirahisi.

Mafuta yanayoweza kutumika hapa ni kama vile;
 ๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Almond  oil
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Coconut  oil
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Black Castor  oil
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Avocado  oil
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️ Black  seed oil
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Carrot oil

Mara zkte kwenye products za nywele hasa mafuta  ni kujaribu na kujaribu mpaka mwisho kuja kupata kitu gani nywele zako zinakubali na kuzingatia. Zingatia sna  nywele yako inakubali mafuta gani vizuri, pia kama unamba, miwasho au vidonda usitumie.

JINSI YA KUANDAA
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Chemsha  maji ya moto
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️ Chukua  mafuta weka kwenye chombo cha bati kisha kalisha juu ya maji ya moto

NB: Unaweza kuchanganya mafuta mawili tofauti halafu ukayapasha  moto na kutumia.
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Hakikisha  nywele yako ni safi kata mistari anza kupaka kisha massage vzr kichwa chote.


FAIDA ZA HOT OIL TREATMENT
๐Ÿ‘‰Kuongeza  mzunguko wa damu kichwani
๐Ÿ‘‰Kupunguza  ukavu kichwani  maana matundu  ya nywele yatafunguka kupelekea mafuta na maji kupenetrate vzr.
๐Ÿ‘‰Nywele  kuwa imara zaidi
๐Ÿ‘‰Kupunguza  nywele kujikunja sana au kujifunga

Unaweza kufanya hot oil treatment mara moja kwa mwezi, lakini ni vizuri kufanya  kila wiki  baada ya kuweka steaming wakat nywele bado safi halafu una massage Kwa nusu saa.

Tuesday, June 30, 2020

86. JINSI YA KUKUZA NYWELE KWA HARAKA


-Zifanye  nywele zako zisiwe kavu sana ( moisturize).

Tumia maji, moisturizing conditioner, au kwa kuchanganya nusu mafuta ya mzaituni (olive oil) na nusu mafuta ya nazi (coconut oil), au unaweza kutumia vyote kwa mpangilio sahihi.

-Fikiria kutumia protein conditioner. 
Hizi huzifanya nywele za aina flani kuwa imara na pia inaweza kuwa na madhara kwa kuzifanya nywele ziwe kavu na kukatika kiurahisi. usiiache kwenye nywele kwa muda lefu tumia kama ilivyo elekwezwa.

-Paka  mafuta mazito (to seal in moisture, kama vile Black castor oil or Shear butter)
Ngozi yako ya kichwa inapo kuwa kavu tumia mafuta ya nazi kupaka ngozi yako kwa kutumia ncha ya kidole chako. acha kupaka unapo kuta mba kwasababu mafuta hayo yanaweza kuwa chakula kizuri cha fangasi hao.Kama una mba paka mafuta mara  moja kwa wiki au tumia mafuta ya moto.

Pia tumia  neutralizing shampoo kuondoa  mafuta na madawa yote ulio tumia kwenye nywele zako.

NJIA YA PILI

-Tumia  vitamins
Vitamin supplements zinakupa virutubisho vinavyo kusaidia kukuza nywele zako


- Kula vyakula vya protein.
Vyakula vya protein kama vile nyama, maziwa, maharage ya soya, maparachichi, na mbegu za maboga.

Sunday, June 28, 2020

85. JINSI YA KUREFUSHA NYWELE KWA HARAKA

Kama wewe ni mwafrika au una asili ya afrika basi tambua kuwa nywele zetu hukuckua muda mrefu sana kurefuka. Lakini zipo njia zinazo weza kukusaidia kurefusha nywele zako kwa haraka. Leo tujifunze kidogo njia mojawapo ya kukuza nywele zako kwa haraka zaidi.

NJIA YA KWANZA
Kuosha na matibabu.

-Tambua aina ya nywele zako
Unaweza kutambua aina ya nywele zako kwa kuwaona wataalamu wa saloon, kujua aina ya nywele zako itakusaidia kuchagua matibabu sahihi na products  sahihi kulingana na nywele zako.

-Osha nywele zako pale tu inapo hitajika.
Usipende kuosha nywele zako mara kwa mara kwani unaziondolea mafuta ya asili. jaribu kuosha nywele zako mara moja kwa wiki au mara moja kwa wiki 2 kama huwa zinakatika katika.Tumia  shampoo ambayo haita zaicha nywele zako zikiwa kavu sana. Ili kupunguza  madhara ya bidhaa unazotumia zioshe  nywele zako kwenye maji ya vuguvugu kisha zisuuze kwenye maji yaliyo poa.

-Ziache  nywele zako zikauke zenyewe
Kama unatumia hair blower kukaushia nywele zako ni vyema utambue kwamba joto kutoka katika blower linaweza kukusababishia madhara katika nywele zako na kuzifanya zikatike kabla hazijafikia urefu unao uhitaji. Badala  yake unaweza kuzikusanya nywele zako na kuzifunga kitambaa na uziache zikauke usiku kucha, Au unaweza kuzikausha kwa kutumia taulo.
-Tumia conditioner kila  unapo osha nywele zako.
Shampoo inaondoa mafuta ya asili yaliyopo kwenye nywele zetu, badala yake unaweza kurudisha mafuta hayo kwa kutumia conditioner inayo faa kulingana na nywele zako.

-Paka mafuta ya nywele kila siku.
Ukipaka mafuta ya nywele unazifanya nywele zako ziwe laini  hii itakusaidia kuzuia zisikatike.
Tumia mafuta ya maji (kimiminika) kama vile;
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️ Black castor oil
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Lavender oil
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Avocado oil
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Olive oil
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Coconut oil nk
Zifunge  nywele zako na kitambaa kuzisaidia zishike mafuta.

ITAENDELEA......

84. JINSI YA KUTUNZA NGOZI YA KICHWA

Mara nyingi tumekua tumeongelea jinsi ya kutunza nywele, leo tutaangalia  jinsi ya kuwa na ngozi ya kichwa yenye afya (Healthy Scalp)

๐Ÿ€Nini ufanye ili uweze kumaintain ngozi yenye afya na kama ngozi yako ina afya ni rahisi nywele kuota vizuri na nywele kuwa na muonekano mzuri hivo msingi mzuri wa utunzaji wa nywele unaanzia kwenye ngozi yako  ya kichwa itunze vizuri sio kila mafuta unatumia unaharibu ngozi yako cha Kwanza,

NINI UFANYE
๐Ÿ‘‰Kula vizuri na kunywa  maji kwa wingi
๐Ÿ‘‰Epuka kuosha mara kwa mara nywele yako au mara chache wengine huosha mara moja hupelekea mrundikano wa uchafu.
๐Ÿ‘‰Tumia  natural products (zisizo na viambata sumu) kwa nywele yako lakini pia unaponunua zingatia ingredients zillio tumika kutengenezea hizo products na muda wake wa kuisha (Expiry date)
๐Ÿ‘‰Epuka  rangi za nywele na hata dawa za nywele zinadhoofisha sana nywele
๐Ÿ‘‰Epuka  kusuka misuko hatarishi au kukazwa sana lakini pia massage kichwa chako mara kwa mara.


๐Ÿ€Lakini pia kama unatatizo la miwasho mba wasioisha basi tumia steaming ya  tangawizi kitunguu swaumu na kitunguu maji saga pamoja unaweza changanya  na asali ukaweka kichwan kwa tumia hata mara 4 kwa miezi 2 (Hili somo lilishaelekezwa kwenye posts zilizopita๐Ÿ‘‰๐Ÿป๐Ÿ‘‰๐Ÿป

๐Ÿ€Au unaweza kuoshea apple cider vinegar unachanganya na maji vijiko viwili vya maji kwa kimoja cha apple cider vinegar (Hili pia lilishaelezewa)

๐Ÿ€Pia unaweza kuosha nywele ukakata mistari kisha ukascrub kichwa chako kisha ukaosha tena hapa nazungumzia scrub ya sukari ukachanganya na mafuta ya castor oil  au scrub ya sukari, kahawa na asali unachanganya kisha ukascrub kichwani ukimaliza iyache ikae hata dakika 5 kisha osha. Scrub ni nzuri sana maan itasugua vzr mba watoke na inatibu miwasho kwa haraka pia hii njia sio steaming kwa nywele zako hivo unaweza ukaamua ufanye lini na ukitumia hii njia utatakiwa kuweka tena steaming kama kawaida.

Friday, June 26, 2020

83. JINSI YA KUTUNZA NYWELE ZENYE DAWA



Mara nyingi tumekua tukiongelea nywele za asili (Natural hair) lakini sio watu wote wenye passion (uvumilivu wa kutunza nywele za asili). Hivyo basi leo nitatoa tips kidogo kuhusiana na jinsi ya kutunza nywele zenye dawa (Relaxed hair) ili ziweze kupendeza vizuri.

Nywele zenye dawa ni nywele ambazo mwanzo zilikua za asili lakini zikaongezewa vilainishi (relaxers), hivyo kurudi kuwa natural kutoka kwenye nywele za dawa ni either ufanye transition (kuacha nywele ziotee huku ukipunguza zenye dawa juu) au kufanya big chop (kunyoa kabisa nywele zote na kuanza upya).

Tuangalie vitu vya msingi vya kuzingatia ili uwe na nywele nzuri zenye dawa
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Hakikisha unachagua dawa ya nywele inayoendana na nywele zako. Hapa pemdelea sana kutumia dawa za box na sio za kopo maana dawa za kopo ni kali mno zinaweza kuleta madhara ndani na nje ya kichwa ndani ya muda mfupi. Na dawa za nywele zinawekwa chini tutu kwenye maotea ya nywele usiweke juu.

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Lazima  upange muda wa kuweka nywele dawa. Dawa inatakiwa kuwekwa mara tatu au mbili tu kwa mwaka. Kama nywele zako ni laini basi unaweka kila baada ya miezi 6 na kama nywele zako ni ngumu sana basi kila baada ya miezi minne ndio unaweka dawa. Usiweke mara kwa mara; kumbuka hizo ni chemicals na zinaenda kukutana na ngozi ya kichwa directly. Pian wengine huweka dawa baada ya miezi mitatu vyote inategemea na aina ya nywele zako.

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Suka  mitindo rafiki na nywele zako usipende kusuka tu kila mtindo chagua mitindo ambayo haitakata nywele zako.

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Hakikisha  unaosha nywele zako mara  kwa mara. Angalau  mara  3 au nne kwa mwezi. Nywele zikijaa uchafu haziwezi kupumua vizuri hivyo zitakua kwa kusua sua sana.

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Tumia  mafuta rafiki na nywele zako. Mafuta  yenye uwezo wa kutunza unywevu na kuzuia nywele kukatika. Mafuta hayo ni kama vile Black castor oil, Coconut oil, Olive oil, jojoba oil nk

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Punguza  matumizi ya moto kwenye nywele..  Mfano .kupasi nywele au kukausha nywele na dryer. .Hii  hufanya nywele kutokuwa na nguvu hivyo kuwa dhaifu sana hivyo unashauriwa usifanye mara kwa mara.

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Tumia kofia ya satini au kitambaa cha safini wakati wa kulala (usilale kichwa wazi au na kitambaa kigumu); Hii inasaidia  nywele kufyonza mafuta ipasavyo na  kumaintain Ph

82. MAKOSA UNAYOFANYA WAKATI WA KUOSHA NYWELE ZAKO- PART 2



๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Kutokuosha na kurudiaRinse & Repeat

Ni muhimu sana kuosha nywele na kurudia. Na hii ni muhimu zaidi kwa wale wenye nywele ndefu. Kama una nywele fupi au ndogo kabisa si lazima kwako kuosha na kurudia. Baada ya kuwa umesugua ngozi ya kichwa “scalp” kwa dakika tatu, ni muda wa kuosha nywele. Ukishaosha inafuata hatua ya pili ya uoshaji wa nywele. Unatumia shampoo kama kawaida. Kwenye hatua hii utaweka msisitizo zaidi kwenye nywele zenyewe kwakuwa tayari ngozi ya kichwa ulishashughulika nayo kabla. Mara hii weka msisitizo zaidi kwenye kuosha nywele zako na hakikisha hakuna nywele inayoachwa bila kupata shampoo kuanzia kwenye mzizi mpaka kwenye ncha.
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Kutokutoa  shampoo vizuri kwenye nywele.
Baada ya kurudia kuosha nywele kwa mara ya pili kinachofuata ni kutoa shampoo kwenye nywele.
Watu wengi hawatoi shampoo vizuri kwenye nywele, na hii huzifanya nywele kubaki na shampoo ambazo zinasababisha nywele kubaki na vitu vyeupe vyeupe “build-ups” na nywele pia kutosafishika vizuri. Hivyo inasisitizwa kutumia muda na maji ya kutosha kutoa shampoo na kuhakikisha imetoka kabisa kwenye nywele ili nywele zako ziwe zimesafishika vizuri.
Yapo makosa mengi sana ya utunzaji wa nywele yakianziwa na uoshaji wa nywele. Ila tukianza kuyasahihisha baadhi ya makosa tuliyoyaelezea hapo juu na kuanza kufuata utaratibu mzuri wa uoshaji wa nywele naamini sote tutakuwa tumeanza safari nzuri ya kuelekea kuwa na nywele nzuri na zenye afya!

81. MAKOSA UNAYOFANYA WAKATI WA KUOSHA NYWELE ZAKO-PART 1


Leo utajifunza namna sahihi ya kuosha nywele ili uziache nywele zako zikiwa safi kana kwamba umeziosha kwa mtaalamu wa saluni. 
Wote  tunaosha nywele ila haitakushangaza ukisikia kwamba uoshaji wa nywele zako si sahihi. Wengi wetu tumekuwa tukifanya makosa kadhaa wakati wa kuosha nywele. Baadhi yetu hatutumii muda wa kutosha kusugua scrub” ngozi ya kichwa “scalp”, hatuoshi vizuri na baadhi pia hatutumii conditioner. Na haya ni baadhi tu ya mambo ambayo tunakosea wakati wa kuosha nywele.

Yafuatayo ni makosa makubwa matano watu wengi huyafanya wakiwa wanaosha nywele
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Kutolowanisha nywele vizuri.
Watu wengi hawaloweshi nywele zao vizuri kabla ya kupaka shampoo. Ni muhimu kulowesha kila unywele kwa maji kabla ya kupaka shampoo. Kila nywele inahitaji kuloweshwa, kisha ipakwe shampoo ili ipate kutakata vizuri.
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Kutumia shampoo nyingi sana au kidogo sana.
Wote  tunafahamu kwamba kitu chochote kikizidi kina madhara au hakitaleta matokeo mazuri. Tunatakiwa kutumia kila kitu kwa kiasi. Si kwa wingi sana na si kwa uchache sana. Kanuni hii pia inatumika kwenye upimaji wa kiasi cha shampoo cha kutumia wakati wa kuosha nywele.
Kutumia shampoo nyingi kunaweza kukufanya usiweze kuipata nywele na kuisafisha vizuri kutokana na kuzidiwa na povu jingi sana. Na kutumia shampoo kidogo kutafanya nywele zako zisitakate vizuri. Pima shampoo kiganjani kwako, kiasi cha wastani kulingana na ukubwa na wingi wa nywele zako, kwa kutumia vidole paka shampoo kwenye nywele zako ulizozigawanya kwenye makundi manne. Paka kuanzia kwenye ngozi ya kichwa “scalp” kuja kwenye ncha ya nywele
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Kutotilia  maanani zaidi ngozi ya kichwa.
Kama  umeshawahi kufanyiwa shampoo kitaalam saluni bila shaka unajua ni muda kiasi gani huwa wanautumia kwenye ngozi ya kichwa. Kusugua ngozi ya kichwa ni hatua ya msingi zaidi kwenye mchakato wa kuosha nywele.
Watu wengi hawatumii muda wa kutosha kusugua ngozi zao za kichwa. Tunatakiwa kusugua ngozi zetu za kichwa kwa walau dakika tatu. Bila kujali urefu au aina ya nywele zako unachotakiwa ni kusugua ngozi yako ya kichwa. Na unatakiwa kufanya hivyo kwa kutumia vidole na sio kucha kwa muda usiopungua dakika tatu.

INAENDELEA....

Thursday, June 25, 2020

80. JINSI YA KUOSHA NYWELE


๐Ÿ€Utaratibu wa kuosha nywele unaweza kuchangia nywele kukatika au kuto kukua vizuri hivo kabla sijaanza kufundisha steaming ni nini au protein ni nini basi tujifunze kuosha nywele zetu kwanza.

HATUA
๐ŸซStep 1: Kama umesuka nywele fumua kisha detangle(kuachanisha vizuri kwa vidole ama chanuo pana)baada ya kuachanisha vizuri unaweza ku tumia detangle cream, spray au leave in conditioner( sio muhimu sana) kisha suka mabutu makubwa ama twist kama una nywele ndefu Kama una nywele fupi acha.

๐ŸซStep 2:  apply mafuta ya kukuza nywele(growth oil) kama coconut oil, shime oil, , jojoba oil, castor oil, black seed oil, avocado oil au essential oil make sure ni kimiminika step hii inasaidia ngozi isikaukiwe na mafuta na ina act kama pree_poo(pree_shampooing) na unapaka zikiwa hivo zimesukwa.

๐ŸซStep 3: osha kwa free sulphate shampoo hapa ziko nyingi inategemeana na brand gani utanunua osha vizuri ukiwa umezisuka kisha kausha kwa khanga au shati na kama utatumia taulo basi usisugue kalisha tu kichwani, pia kwenye kuosha waeza oshea maji ya vugu vugu kulingana na hair porosity yako.

๐ŸซStep 4: weka steaming yako au protein treatment kulingana na ratiba yako vaa mfuko wa plastic kisha funga kiremba juu upate joto vizuri kama steaming yako ni ya saa moja,nusu saa au dakika 45 kaa mda huo  kisha toa, osha kwa maji ya baridi kisha kausha.

๐ŸซStep 5: paka mafuta yako kisha paka leave in conditioner au paka leave in cinditioner( kama bamia,  alovera, flaxseed au za dukani nitakuja kufundisha) kisha mafuta.

๐ŸซStep 6: suka nywele yoyote kama ya uzi au ya mkono, pia pendelea kulala na kitu kichwani hususani iwe na material ya satini.

79. JINSI YA KUFANYA NYWELE KUWA NA UNYEVU

Kama ambavyo mwili unahitaji maji kuendelea kunawiri vivyo hivyo nywele zetu zinahitaji unyevu ili kuendelea kuwa nzuri na zenye afya. Kuna niia ambazo zimezoeleka  kufanya nywele kuwa na unyevu; Hivyo wewe kama mtu unaetunza nywele unatakiwa ujue aina ya nywele zako na njia gani ya kuhifadhi nywele inkubalika na nywele zako.
Njia hizo zinaoneshwa vizuri kwenye picha hii ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ


C= Cream (Unaweza tumia Shea butter au  Mango butter)
O=Oil (Hapa tunatumia carrier oils kama vile Black Castor oil, Coconut oil, Olive oil, Jojoba oilnk)
L=Leav in Conditioner/Water based conditioner (Unaweza tumia ambayo inaendana na nywele zako, ila ambayo imezoeleka ni brand ya Cantu au Antie Jackies Leave in conditioners japo unaweza tumia ya asili ya kutengeneza mwenyewe nyumbani kama Vile Gelly ya Aloevera au ya bamia.

Wednesday, June 24, 2020

78. KANUNI 10 ZA KUWA NA NYWELE NZURI


๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️ Jua jinsi ya kuchana nywele zako kwa usahihi

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Jua jinsi ya kufumua nywele zako kiusahihi na jinsi ya kuzitunza wakati umefumua ili kuzuia kukatika.

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️ Jinsi ya kubana na kusuka nywele pamoja na kuchagua mitindo rafiki kwa ajili ya nywele

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Treatments za  kufanya katika nywele zako
  - Steaming(deep conditioner)
  -Protein treatment
  -Hot Oil treatment
  -Hair mask
  -Leave in conditioner

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️ Jinsi ya kupaka mafuta kichwani

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Vitu vya msingi vya kuwa navyo kabla haujaanza kuhudumia nywele zako

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Vitu vya kuepuka katika kuhudumia nywele zako

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Kwanini umeamua kuwa na nywele za asili

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️ Una malengo gani na nywele zako

๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️UVUMILIVU

Tuesday, June 23, 2020

77. JINSI YA KUKUZA NYWELE KIRAHISI

Leo tuangalie mtu anawezaje kukuza nywele zake za asili kirahisi kabisa kwa kutumia vitu vya kawaida ambavyo vinapatikana jikoni kwa kila mtu.

MAHITAJI
-Kitunguu maji
-Tangawizi
-Kiazi mviringo
-Olive oil (Mafuta ya mzeituni)
-Mafuta ya nazi (Cococnut oil)
-Mafuta ya mnyonyo (Black Castor oil)
-Asali kidogo
-Kiazi mviringo

Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo husaidia kukuza nywele na kuzuia MBA kwenye nywele.

JINSI YA KUANDAA
 -Chukua kikwaruzio cha nyanya / karoti (grater) halafu chukua  kitunguu chako kwaruza pale upate ule uji uji wake
-Chukua tena tangawizi na kiazi kwaruza/kwangua upate ule uji uji baada ya hapo chukua chujio au kitambaa kisafi changanya huo mchanganyiko wako wote then chuja/kamua ili kupata juice  yake
-Ongeza vingine vyote vilivyobaki na uchanganye vizuri (mafuta unaweza kidogo kidogo tu)

NB: Unaweza kutumia blender kusaga vitu vyako vyote kwa pamoja halafu mwisho utachuja upate maji maji yake

JINSI YA KUTUMIA HUO MCHANGANYIKO WAKO
-Chukua chupa  weka hiyo juice iliyopatikana
-Funua nywele zako na uzipshe vizuri na shampoo isiyo na viambata sumu
-Paka  huo mchanganyiko wako kweny ngozi ya kichwa kwa kutumia vidole na sio kutumia kucha  paka kichwa mpaka kienee chote
-Chukua mfuko wa plastic au makofia   ya plastic vaa kichwan kwa muda wa saa moja au unaweza kulala nayo usiku kucha
(pia unaweza kukaa kwenye steamer kwa dakika 20 hadi 25 ili kupata joto vizuri)
-Baada ya hapo osha nywele zako vizuri na maji ya kawaida tu.

JINSI YA KUTUMIA MAFUTA
-Chukua mafuta ya nazi, ya mnyonyo na mzeituni kiasi kidogo changanya alafu yapashe kidogo yapate joto (Hot oil treatment)
- Paka vizur kwenye nywele kuanzia kwenye ngozi ya kichwa halafu kaa  lisaa limoja halafu osha  kwa kutumia shampoo hakika utazifurahia nywele zako.
-Mwisho paka mafuta yako ya joto la kawaida na hapo uko tayari kubana style yoyote au kwenda kusuka.

Friday, June 12, 2020

76. JINSI YA KUZUIA NYWELE ZAKO KUKATIKA

Henna ina matumizi mengi sana; leo tuangalie jinsi gani unaweza tumia henna kwa matokeo mazuri zaidi.
Leo tuangalie jinsi gani unaweza kutumia henna kuzuia nywele kukatika hasa ncha.

MAHITAJI
Vijiko vi 2-3 vya chakula vya henna
•Parachichi moja la wastani
•Yai moja (La kienyeji)
•Maji kidogo kama mchanganyiko utakua mzito sana

JINSI YA KUTUMIA
-Osha nywele zako vizuri na shampoo isiyo na viambata sumu
-Kausha kidogo nywele zako kuondoa maji yanayochuruzika
-Changanya vitu vyote upate uji mzito wastani, -Paka kichwani kuanzia kwenye ngozi mpaka ncha ya nywele zako. -Kaa na mchanganyiko huo angalau masaa mawili kisha osha.

KUJAZA NYWELE NA KUFANYA ZING’AE
MAJITAJI
•Chai ya rangi nusu kikombe
•Maji ya limao Kijiko cha chakula kimoja
•Yai au maziwa ya mgado

JINSI YA KUTUMIA
Loweka Henna usiku mzima kwenye chai ya rangi. asubuhi unapotaka kutumia ongezea viungo vilivyobakia. Paka dakika ishirini (20) Kabla ya kuoshwa nywele.

HENNA KWA AJILI YA NYWELE KAVU
Changanya Henna, mafuta ya nazi kiasi na Olive oil (mafuta ya mzaituni) uwe na uji mzito kiasi. Paka kichwani kaa nao lisaa kisha safisha.

NB: Hizi  treatment unaweza kufanya kwa nywele natural na zinye dawa, hakikisha unatumia Henna ya asili isiyotiwa kemikali.

Wednesday, June 10, 2020

75. JINSI YA KUTUMIA HENNA KAMA CONDITIONER

MAHITAJI
-Vijiko vinne vya chakula vya hena
-Nusu kikombe cha chai ya rangi iliyokolea majani
-kijiko kimoja cha chakula cha juice ya limao
-maziwa ya mgando (yogurt/mtindi)

JINSI YA KUTUMIA 
•Osha nywele zako vizuri kwa kutumia shampoo isiyo na viambata sumu
•Kausha nywele zako kidogo ili kuondoa maji yanayochuruzika
•Changanya vitu vyako vyote pamoja
•Paka mchanganyiko huo kichwani
•Kaa nao angalau lisaa.
•Baada ya hapo osha nywele zako na maji ya kawaida mengi
•Halafu unaweza fuata LOC Method kama kawaida.

Hii treatment italainisha nywele kwa maana ya kuzinyoosha na kuzipa mng'ao mzuri.

74. FAIDA ZA KUTUMIA HINA (HENNA) KWENYE NYWELE


Henna (Hina) inasaidia katika kubalance  hali ya kichwa kwa maana ya pH na kusaidia kuondoa muwasho wa ngozi ya kichwani.
•Inasaidia  nywele kukua kiusahihi
•Inapunguza  kukatika kwa nywele na kasi ya mvi kuota kwa wale wenye asili ya mvi au wenye umri mkubwa
•Inaweza kutumika kuzipa nywele zako rangi na mng'ao wa tofauti kadri unavyoitumia (Hair dye)
• Pia unawez  kuitumia Henna Kama conditioner (Tutaangalia kwenye somo linalofuata)

Tuesday, June 9, 2020

73. JINSI YA KUTUNZA NYWELE ASILIA (NATURAL HAIR)


Leo katika somo letu la urembo ningependa kuangalia katika utunzaji wa nywele bila ya kujihusisha na matumizi ya madawa ya kemikali ambayo yamesababisha kwa kiwango kikubwa matatizo katika ukuaji wa nywele kama nywele kukatika,kunyonyoka,kupooza katika ukuaji n.k

Hinw ni moja kati ya mimemq ambayo watu wengi hasa wanawake huitumia katika kujiremba hasa kujichora bila kutambua kuwa mmea huo unaweza tumika katika utunzaji wa nywele zao kwa kasi kubwa. Leo tutaangalia jinsi ya kutumia hina katika utunzaji wa nywele.

MAHITAJI
•Hina vijiko vitatu vya chakula
•Kipande cha ndimu au limao
•Maji ya chai kiasi kidogo
•Gloves mbili mpya

JINSI YA KUANDAA
Vaa gloves ili mikono yako isiharibiwe na hina
•Changanya hina na viungo vingine vyote hakikisha haiwi nyepesi sana wala nzito sana
•Gawa nywele zako katika mafungumanne, kisha paka hina yako kwa uangalifu, hakikisha kila fungu limekolea vizuri na usichafue uso wako
•Baada ya hapo unakaa nayo ukiwa umevaa mfuko wa plastic au kofia ya kulalia kwa muda usiopungua lisaa
•Zikiwa tayari unaosha nywele zako vizuri na kukausha kwa kitambaa cha cotton au tshirt
•Baada ya hapo unaweza kuziweka nywele zako katika mtindi wowote ule unaopenda baada ya kupaka mafuta mazuri yasiyo na chemicals (Black castor oil, jojoba oil, coconut oil or olive oil)

ITAENDELEA...
-Matumizi mbali mbali ya hina, kama vile kung’arisha nywele, kama stemaing, kukuza na kujaza nywele nk

72. MATUMIZI YA MLONGE KWENYE NYWELE


Mlonge ni mmea ambao unafaida nyingi sana katika mwili wa binadamu na unatumika sehemu mbalimbali duniani, hii inapelekea kuwa na majina mengi sana, baadhi nitayataja hapo chini๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
✅Moringa Oleifera
✅Drumstick tree
✅Miracle tree
✅Ben oil tree
✅The horseradish tree
Na mengine mengi sana kulingana na eneo au nchi ambayo mtu yupo.
Mlinge unatumika katika bidhaa mbali mbali za afya na za nywele; Leo nitaongelea tu kuhusiana na umuhimu wake kwenye nywele.

Majani ya Mlonge (Moringa leaves) yanapendwa sana na watu wanaotunza nywele zao kwa sababu yana madini na vitamins za kutosha kurutubisha nywele vizuri.
Mlonge una;
•Vitamin A, E na B
•Calcium, Potassium, Zinc na Iron

FAIDA ZA MORINGA LEAVES
Yanaimarisha hair follicles
Yanaimarisha mzunguko wa damu, virutubisho na oxygen kwenye scalp
•Improve hair growing process (inasaidia ukuaji mzuri wa nywele)

JINSI YA KUANDAA
•Chukua majani kadhaa ya mlonge yaoshe vizuri yawe masafi
•Baada ya hapo weka kwenye sufuria, ongeza maji kidogo acha vichemke kwa muda wa dakika 5
•Acha maji yapoe, ongeza mafuta kidogo kisha uwe unaspray kwneye nywele mara kwa mara na baada ya kuspray seal in moisture.

Monday, June 8, 2020

71. MUAROBAINI (NEEM LEAVES) KWA AJILI YA NYWELE

Wote tunajua katika jamii zetu muarobaini/neem ni dawa nzuri sana ya asili, lakini leo sitakngelea kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali ya mwili; Ila nitaongelea jinsi gani muarobaini unaweza tumika katika kukuza nywele zetu (hasa nywele za asili).

FAIDA ZA MUAROBAINI KWENYW NYWELE
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Ni anti-bacterial; Na hii huenda kwenye scalp moja kwa moja hivyo inasababisha kupambana vyema na magonjwa nyemelezi ya kichwa kama vile mba, vidonda, kuwashwa nk.
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Inasaidia kuondoa infections mbalimbali kwenye kichwa kama zilikuepo na pia kulinda ngozi ya kichwa isipate infections kama haijawahi kupata.
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Kusaidia nywele kukua kirahisi na kiharaka zaidi, hata kama nywele zKo zilikua hazikui vizuri tumia muarobaini mara kwa mara utaona matokeo yake.

NB: Unaweza kupaka kwenye scalp tu au hata juu (kwenye nywele zote) ina nutrients za kutosha kunourish nywele zako vyema
Pia muarobaini una harufu kali kidogo hivyo kulingana na ulivyo unaweza chagua utumie kama leave in conditioner au kama steaming.

KAMA LEAVE IN CONDITIONER: 
-Unachukua majani kadhaa ya muarobaini, unayasafisha vizuri na kuyaweka kwenye sufuria
-Ongeza maji kiasi kama robo lita tu
-Acha ichemke kwa dakika 5 hivi ikiwa imefunikwa
-Baada ya hapo weka kando yapoe vizuri
-Halafu weka kwenye spray bottle yako, ongeza na mafuta kidogo kisha utakua unaspray kila ukihisi nywele kavu (wakati unataka kuzipa nywele unyevu)

KAMA STEAMING:
-Chukua majani kadhaa yasafishe vizuri
—Baada ya hapo weka kwenye blender ongeza na maji kisogo halafu saga
—Ukishasaga toa kwenye blender chuja na upate maji maji ya kijani
—Ongeza asali na mafuta yoyote ya nywele (Carrieer oils - mafuta ya mnyonyo, olive oil, coconut oil)
-—Nywele zikiwa safi paka mchanganyiko wako kwwnye nywele
—Unaweza  kucaa mfuko wa plastic, shower cap au ateamer kwa dk 30 hadi saa 1
—Baada ya hapo osha nywelw zako vizuri ili kuendelea na process nyingine kama vile LOC Method
-

Sunday, June 7, 2020

70. TUJIFUNZE ZAIDI KUHUSU DREADS (DREADLOCKS)


Dreadlocks, ni aina ya nywele ambayo ina historia kubwa kwa mwanadamu kabla ya style yoyote ya nywele, ni style inayotumika kiimani mfano imani ya Uhindi (Saddhus), Some of Tibetian Buddhists (Ngagpas of Tibet), Uyahudi (Nazarines peoples), Hamitic people of North Africa, Watakatifu wa Ethiopia na Oromos wa Ethiopia, Wasemitic, Wamisri wa zamani, Watakatifu wa Spartan wa ugiriki, na Kwenye uislam kuna wasufi wanaitwa Qalandariala (wana  natural dreadlocks) na Rastafarians (katika sects zote za Orthodox, Twelve tribes of Judah, Bobo Shanti na Spirituals). Pia kuachana na Imani imekuwa ni style kuonyesha jinsi unavyoheshimu nywele zako za asili (Your  natural hair)(Kwa Non-Africans and Africans)

Ushahidi wa kisaikolojia  wa kale unaonyesha aina hii ya nywele kiimani imeanza kutumika miaka kati ya 5000BC - 4500BC na ina umuhimu mkubwa  sana katika imani nyingi.

Kwa miaka ya sasa watu wamesahau heshima yake, ila wapo watu ambao wanapenda dreadlocks na wanazo, wanazitunza na kuzijali bila matatizo yoyote na wakiendelea kufanya shughuli zao za kimaendeleo (Sizungumzii wahuni wa mitaani). Pia wapo wengine wanazo kwa sababu ya Imani na wengine kwa sababu ya fashion.

TUTAENDELEA NA JINSI YA KUTUNZA DREADLOCKS


Monday, June 1, 2020

69. STEAMING NZURI KWA NYWELE ZISIZO NA DAWA

MAHITAJI
๐Ÿงš‍♀️Parachichi 1 kubwa
๐Ÿงš‍♀️Ndizi moja iliyoiva vizuri
๐Ÿงš‍♀️Yai 1 la kienyeji
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Asali kijiko kimoja
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Mafuta (Castor oil, jojoba oil or coconut oil) kijiko kimoja

JINSI YA KUANDAA
-Andaa ndizi na parachichi vizuri kisha weka kwneye blender
-Saga vizor mpaka zilainike vizuri kuepuka kubaki na particles kichwani
-Ongeza asali, mafuta pamoja na yai kisha blend tena vizuri
-Baada ya hapo osha nywele zako vizuri na shampoo isiyo na viambata sumu
-Kausha nywele kidogo kuondoa maji yanayotiririka kisha paka steaming yako kuanzia chini kabisa ya nywele (kwenye shina) hadi juu
-Hakikisha nywele zote zimepata steaming
-Vaa kofia ya plastic (zile za kuogea) kwa dakika 45 au kaa kwenye steamer kwa dakika 20 tu. Hii inafanyika kuongeza joto ili steaming iweze kuingia vizuri kwenye nywele.
-Baada ya hapo osha vizuri na maji ya baridi (kufunga vitundu vilivyofunguliwa na joto)
-Halafu utaendelea na LOC Method kama kawaida

FAIDA ZA STEAMING HII
-Kulainisha nywele na kuzuia zisijifunge funge
-Kung’arisha nywele
-Ni chakula cha nywele hivyo kufanya nywele kukua vizuri
-Kuondoa mba, miwasho nk kwa sababu ya asali ambayo ni antifungus.

NB: Kwa matokeo mazuri fanya hii mara mbili kwa mwezi๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

NYWELE NZURI NI MATUNZO


Sunday, May 31, 2020

68. NINI UFANYE ILI NYWELE ZAKO ZIKUE VIZURI?

๐Ÿงš‍♀️Kwanza kabisa unapaswa kuzikubali nywele zako na kuzipenda , jambo hilo litapelekea mahusiano mazuri, kuelewa tatizo la nywele zako na kuanza kuchukua hatua taratibu ya kuzipatia uvumbuzi tatizo hilo.
๐Ÿงš‍♀️Pili, unapaswa kufanya usafi wa kina wa ngozi na nywele zenyewe kwasababu endapo nywele zitaachwa chafu, basi ule uchafu unaziba matundu ya nywele na kuzuia njia kama vile ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata chunusi.
๐Ÿงš‍♀️Tatu, ni kulinda unyevu wa nywele. Pale nywele  zinapooshwa, yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu. Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyoo vizuri na zikikauka zinakuwa kavu sana. Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri, zikafanyiwa ‘condition’ , kwa zile nywele ambazo ni nyepesi na chache pia kuna bidhaa zinasaidia kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Hatua inayofuata ni ya kupaka mafuta kichwani, kwani mafuta yana umuhimu mno katika ukuaji wa nywele na mafuta mazuri ni ya kimiminika kama vile Black castor oil, Coconut oil, Jojoba oil nk  ambayo yamewafaa baadhi ya watumiaji wengi .
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Njia nyingine ni ya kuzichambua vizuri nywele kabla ya kuzichana, hapa mtu anatakiwa kuwa na subira na nywele zake , asifanye haraka haraka kuzichana na ikiwezekana aziloweshe maji kidogo halafu ndipo azichane kwa chanuo kubwa lenye upana wa kutosha (wide toothed comb) ili kuzipa afya na kuepuka kujiumiza wakati wa kuzichana.
NB: Mtu anayetunza nywele za asili anatakiwa kupunguza matumizi ya moto kama vile pasi ya nywele, dryers na vingine kama hivyo. Nywele zinatakiwa zichanwe kawaida na ziachwe zikauke zenyewe kwa hewa bila kuzilazimisha.

Saturday, May 30, 2020

66. JINSI YA KUTUNZA NYWELE ASILIA (NATURAL HAIR)-PART 2



- Kwanza kabisa unatakiwa kuosha nywele zako vizuri kwa kutumia shampoo ambayo imetengenezwa kwa ajili ya natural hair (nywele asili) au kama utatumia shampoo iliyotengenezwa kwa ajili ya nywele zenye dawa basi jaribu kutumia shampoo yenye conditioner. Hii itasaidia nywele zako kuwa laini na kuzuia zisiwe kavu baada ya kuziosha.

- Pili ni kupaka mafuta nywele zako, zifanye nywele zako zivutie kwa kuzipaka mafuta ya maji kama vile mafuta ya nazi, olive oil, jojoba oil au castor oil kwa sababu mafuta haya hulainisha ngozi ya kichwa, kufanya nywele zikue vizuri na kuzuia mba. Mafuta ya mgando hutengeneza mba kwenye nywele za asili kwa urahisi sana tofauti na nywele zenye dawa.

-Pia usisahau kuzifanyia steaming nywele zako kwa mwezi hata mara 2, tumia steaming products kwa ajili ya natural hair au fanya steaming ya yai ni nzuri sana kwa kurutubisha nywele za asili. Mfano; Osha nywele zako na shampoo kisha koroga yai na paka kichwani kwenye ngozi, Vaa kofia ya plastic kwa dakika 45, kisha osha vizuri.

-Kitu kingine ni kuzichana vizuri nywele zako, nywele za kiafrika ambazo hazijawekwa dawa zina asili ya kujisokota au nyingine ni kipilipili hivyo mara nyingi huwa zinafungana, hivyo wakati wa kuchana inabidi uwe mwangalifu zisikatike, tumia chanuo ambalo ni pana na hakikisha umepaka hair lotion (hair moisturizer / pink lotion) kwenye nywele na mafuta ndio uanze kuchana taratibu. Wakati wa kulala jaribu kusuka mabutu na kuvaa kofia ili nywele zisijifunge au kujisokota.

Thursday, May 28, 2020

65. JINSI YA KUTUNZA NYWELE ASILIA (NATURAL HAIR)

Kwa wale ambao tuna nywele asilia ( natural hair) tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo. Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia, karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu.

Katika mada ya leo,nitakwenda kuzungumzia vitu vya kuzingatia ili kuikuza nywele yako asilia kwa haraka zaidi. Je,unazifahamu nywele zako vizuri? Una nywele za aina gani? Zina tabia gani? Zinataka na kupenda nini?

KARIBU UJIFUNZE

- Kuzikubali kama zilivyo na kuzipenda.
Utasikia ..hiki kipilipili changu ni steelwire ya kimataifa, ..hakitikisiki hata upepo wa dunia yote ungevumia pande hizi. Mwingine oh.. nywele zangu kama miti ya mibuyu kichwani…hazishikiki.Tatizo ni kwamba hamjafahamiana vizuri yani wewe na nywele zako. Hata mimi niligombana nazo sana huko nyuma kabla ya kuzielewa vizuri hivyo jambo la msingi la kuzingatia katika nywele zako ni kujenga mahusiano mazuri tu na nywele zako ,zielewe, ukifikia hapo utaanza kuzipatia hata hazitakusumbua.

- Usafi wa ngozi ya nywele na nywele zenyewe.
Nywele zenye afya huanzia kwenye ngozi safi ya nywele. Nafahamu unataka nywele zako zisidumae kwa hiyo zioshe vizuri. Wakati uliopita nilizungumzia kuziosha kwa product zilizo rafiki(Products zisizo na viambata sumu). Ngozi safi ya nywele itasababisha nywele kupata njia ya kujitokeza nje kwa urahisi. Unapoziacha chafu, ule uchafu unaziba matundu ya nywele zako na kuzuia njia, kama ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata machunusi maana uchafu unajaa basi kwa nywele hazitakua vizuri.

-Linda unyevu wa nywele zako
Kila mtu akisikia kiu hunywa maji. Nywele zako zinahitaji kulindwa zisisikie kiu. Unapoziosha,yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu. Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyopo vizuri, na zikikauka zinakua kavu sana. Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri, ukazi-’condition’. Kwa nywele ambazo ni nyepesi na chache, pia kuna product za kuzisaidia ziweze kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.

- Zifahamu nywele zako
Yani hapa ndo shule ilipolalia kabisaa maana ukizijua tu basi utazihudumia kwa usahihi. Unatakiwa kuangalia namna gani nywele zako zinanyonya unyevu. Unajuaje?
Nilishaelezea kwenye posts zilizopita ila leo pia nitarudia kwa kifupi..
๐Ÿงš‍♀️Chukua kikombe,kijaze maji safi (Ukipata glass itakuwa vizuri zaidi)
๐Ÿงš‍♀️Chomoa unywele mmoja kichwani,hakikisha unatoka na kale kamzizi kake keupe keupe hivi.
๐Ÿงš‍♀️Tumbukiza unywele wako kwenye glass yako ya maji hakikisha imeingia yote.
MATOKEO
-Kama ikizama hapo hapo na hainyanyuki tena,basi nywele zako zinanyonya unyevu kwa haraka kabisa.
-Kama inachukua muda kuzama,au haizami kabisa,nywele zako zinanyonya unyevu taratibu au zinanyonya kwa shida .(Wala usihofu,zipo namna ya kuzifanya zinyonye unyevu kwa haraka,tutajuzana.)
Ni kwamba ‘cuticle’ zake zimefunga haswa,ndio maana unyevu au maji haviingii kwa haraka.

๐Ÿงš‍♀️Kwa hiyo ukifanya ‘deep conditioner’ kwa kutumia joto kama la drier lakini uwe moto mdogo sana au ufanye ‘hot oil treatment’ itakusaidia ‘cuticle’kufunguka na unyevu kupita.
๐Ÿงš‍♀️Mbadala,unaweza baada ya kuosha suuza na maji ya vuguvugu halafu weka mafuta ya kimiminika.Inasaidia sana.

Je wewe una nywele aina gani? Tukutane kwenye comments๐Ÿ˜˜

KUMBUKA: NYWELE NZURI NI MATUNZO NA HAKUNA NYWELE ZINAZOKATAA MATUNZO MAZURI

ITAENDELEA....

Monday, May 25, 2020

64. JINSI YA KUNYOOSHA NYWELE BILA KUTUMIA MOTO

Picha hii inaonesha tofauti kati ya nywele iliyoharibika (Damaged hair) na nywele nzuri zenye afya (Healthy hair)


Katika utunzaji wa nywele asili, adui mmojawapo anaeweza kuziharibu nywele zako na kufanya usipate matokeo mazuri na kufanya nywele za zisipemdeze ni matumizi ya moto; iwe katika kukausha, kunyoosha au kuset. Kama unataka nywele ndefu za asili, inabidi uanze kujifunza jinsi ya kurefusha nywele zako na kutunza nywele zako. Leo nakupa siri kadhaa za kuzingatia ili kukuza nywele zako kiusahihi zaidi na kupata matokeo unayoyapenda.

 – Nywele sio asili ya mtu: Sio lazima uwe ‘point 5’ au mtu mweusi wa Marekani kuwa na nywele ndefu. Watanzania wengi wana nywele ndefu, sema wanajua jinsi ya KUTUNZA NYWELE BILA KUZIHARIBU.

– Usitumie moto kali: Kama unapenda kunyosha nywele zako, usitumie dryer sana kwasababu nywele zako zitakatika. Kama ni lazima utumie blow dryer, tumia setting ya baridi ili nywele zako zinyoke.

– Tumia mafuta mazuri: Tumia mafuta mazuri  ya kukuza nywele zako pamoja na routine nzuri ya kuzitunza nywele zako. Kama unataka nywele ziwe ndefu, paka mafuta kwanza kwemye ngozi ya kichwa,  suka mabutu kabla kulala, na uzipe nywele unyevu mara kwa mara.

-Usiache nywele muda mrefu bila kusuka hii ni kuzuia nywele zisipigwe na upepo sana hivyo kuzuia kujifunga na kukatika pia

 – Tumia shampoo nzuri isiyo na viambata sumu kama salts, paraben na sulphates. Shampoo inasaidia kusafisha ngozi ya nywele ili nywele zako zikue haraka.

KUZA NYWELE ZAKO KIASILI, KIUSAHIHI NA SALAMA ZAIDI

63. JINSI YA KUTUMIA MAJANI YA CHAI KWENYE NYWELE

Majani ya chai yoyote yale yawe ni yale ya kawaida, green tea au rosemary yana umuhimu sana katika ukuaji wa nywele. Wengi hutumia maji yake katika kusuuzia nywele (Wengi huita Rinse out tea); hapa unaweza tumia vitu mbali mbali tutazidi kuviangalia kwenye posts zinazofuta.

FAIDA ZA MAJANI YA CHAI KWENYE NYWELE
-Yanajaza nywele
-Yanang’arisha nywele
-Yanarudisha rangi ya asili ya nywele zako na kuzipendezesha zaidi
-Yanazuia nywele kukatika
-Yanarefusha nywele kama inavotakiwa

NB: Kuna njia nyingi za kutumia maji ya majani ya chai kwenye nywele
1. Unaweza kuchanganya kwenye steaming yako
2. Unaweza kusuuzia nywele zako baada ya kuosha

NJIA YA KWANZA
-Chukua vijiko vitatu vya majani ya chai weka kwenye sufuria safi
-Baada ya hapo ongeza maji nusu lita
-Acha yachemle kwa dakika 5 hadi 10 kisha yaache yapoe kabisa
-Baada ya hapo chuja upate maji ya majani ya chai bila makapi
-Baada ya kuosha nywele na shampoo na kusuuza na maji ya kawaida zimwagie nywele zako maji hayo uliyoandaa (ukimaliza hapo usioshe tena nywele)
-Unaweza endelea kupaka steaming yako uliyoiandaa

NJIA YA PILI
Mahitaji
-Vijiko vitatu (3) vya maji ya chai
-Tui la nazi
-Mafuta ya nywele (Castor oil/Coconut oil)

JINSI YA KUFANYA
-Changanya vyote kwenye bakuli moja
-Paka kwenye nywele zako vizuri
-Vaa kofia ya plastic au kaa kwenye steamer kwa dk 30 hadi 45.
-Osha nywele zako vizuri na maji ya kawaida halafu unaweza suuza tena na maji ya chai uliyokwisha andaa hapo awali.


Sunday, May 24, 2020

62. MAJANI YA MPERA KAMA STEAMING

Katika Post No. 58 tulijifunza jinsi ya kutumia majani ya mpera kama leave in conditioner, pamoja na faida zake kadhaa. Majani ya mpera (guava leaves) ni kati ya kiungo muhimu sana ambacho watu wengi wanaotumza nywele zao kimewaletea matokeo chanya sana. Hivyo hata wewe msomaji kama bado hujajaribu unatakiwa kujaribu iwe ni kuzipa nywele zako unyevu au kama chakula cha nywele.

FAIDA ZA MAJANI YA MPERA 
-Yanafanya nywele zinakua laini
-Yanarudisha rangi ya asili ya nywele na kung’aa zaidi
-Kujaza nywele 
-Nywele zinakua well moisturized

MAHITAJI
-Majani kadhaa ya mpera (10 hadi 20 yanatosha kabisa)
-Mafuta ya maji (Castor oil, coconut or olive oil)
-Asali kiasi

JINSI YA KUANDAA
-Safisha majani yako vizuri ili kuondoa uchafu na takataka zote.
-Yaweke majani kwenye blender na ongeza maji kidogo halafu blend ili kupata juice
-Chuja vizuri mchanganyiko wako ili kupata juice safi
-Ongeza mafuta kidogo na asali kidogo tu (kulingana na kiasi cha juice yako)
-Baada ya kuosha nywele vizuri na shampoo paka steaming yako kichwa kizima kuanzia kwemye shina la nywele
-Baada ya hapo vaa kofia ya plastic au kaa kwenye steamer ili joto liingie vizuri na kufanya steaming iingie vizuri kwenye nywele
-Baada ya dk 45 hadi 1 hour osha nywele zako vizuri kwa maji ya baridi.
-Ukimaliza paka mafuta yako vizuri na Cream (shear butter) halafu unaweza suka style yoyote unayoipenda.

Saturday, May 23, 2020

61. UMUHIMU WA KUFANYA SCRUB YA KICHWA (SCALP EXFOLIATION)

Scalp ni ngozi ya kichwa na hivyo ina tabia kama ya ngozi ya sehemu nyingine za mwili. Kama vile mtu anavokua na dead skin (ngozi iliyokufa usoni) ndio hivyo hivyo anaweza kuwa na dead skin kichwani pia. Ngozi ya kichwa ikizidiwa uchafu iwe kwa sababu ya kuto kuosha nywele vizuri au kuganda kwa mafuta au products nyingine za nywele na kutengeneza kitu kinaitwa Product build up (Pitia post No. 31 & 32) au dead cells kuziba hair roots na kushindwa kuzalisha ngozi mpya ni lazima ukuaji wa nywele zako ufifie.

SCALP EXFOLIATION
Hii inahusisha kutumia njia mbali mbali kuondoa dead skin kichwani, mafuta yaliyoganga (au extra sebum) na mba. Ni muhimu sana katika utunzaji wa nywele uwe na tamaduni ya kufanya scrub ya kichwa ili kupata nywele zenye afya, imara kuanzia kwenye shina na zinazong'aa vizuri. Leo tutaangalia njia rahisi sana ya kufanya scalp exfoliation nyumbani. Ni rahisi, nzuri na inatumia gharama kidogo.

MAHITAJI
-Sukari (natural /brown sugar) vijiko viwili vya chakula
-Kijiko kimoja cha mafuta  (Pure castor oil/coconut oil or olive oil)
-1/2 Apple cider vinegar au Limao
-Scalp massager
-Gloves (ukipenda)

JINSI YA KUTUMIA
-Saga sukari kwa blender au twanga kwa kinu kidogo cha viungo
-Changanya vyote upate kama paste hivi (scrub)
-Tumia vidole vyako au brash (scalp massager) kumassage ngozi ya kichwa ili kufanya scalp relaxation.
-Osha nywele vizuri kwa sulphate free shampoo
-Nywele zikiwa bado zina maji maji kidogo, kata mstari paka scrub kidogo
-Massage scalp yako taratibu kwa dakika 5-10 (tumia scalp massager au vidole)
-Fanya ivyo kwa kichwa kizima
-Baada ya kumaliza osha vizuri kwa maji ya baridi hadi uhakikishe hakuna particles za sukari zilizobaki.
-Baada ya hapo fuata LOC Method (leave in conditioner, oils, cream-shear butter)
-Halafu unaweza suka nywele za uzi (African threading method) ili kunyoosha nywele zako.

USITUMIE MOTO KUNYOOSHA NYWELE ZAKO

NB: Maji ya baridi husaidia kutunza mafuta ya asili kichwani (sebum)


Friday, May 22, 2020

60. UMUHIMU WA KUFANYA MASSAGE YA KICHWA (SCALP MASSAGE)



Scalp kama ilivozoeleka ni ngozi ya kichwa ambayo ndio inapokea nywele changa kabisa kutoka ndani. Scalp massage ina umuhimu sana katika ukuaji wa nywele na hata katika afya kiujumla japo wengi wamekua wakiipuuzia hii step katika utunzaji wa nywele. Scalp massage tunaifanya ili kupunguza tension, kuleta utulivu wa mawazo (relaxation) na kuleta wepesi wa kichwa. Hii inafanyika ukiwa umesuka, umebana nywele au hata ukiwa umeaschia.

JINSI YA KUFANYA
-Paka mafuta kwenye ngozi ya kichwa na kwenye mikono yako
-Sugua taratibu kichwani huku ukiwa umeinamia chini kama inawezekana (hii inachochea mzunguko wa damu kwenye nerves za kichwa) kwa muda wa dk 5.
-Siku ya kuosha nywele (HAIR WASH DAY) unaweza fanya massage na mafuta yako (carrier oils-castor oil, jojoba oil, coconut oil etc) kwa muda wa dk 3 halafu yaache kwenye nywele kwa muda wa dk 15-30 kabla ya kuosha nywele kwa shampoo au conditioner (hii inaitwa PREPOO)

UMUHIMU WA KUFANYA SCALP MASSAGE
-Ngozi ya kichwa ikirelax hata ukuaji wa nywele unakua kama invotakiwa na sio wa kusuasua.
-Ina hamasisha mzunguko mzuri wa damu kichwani
-Inasaidia kulainisha nywele na kufanya products ziingie vizuri na kufanya kazi vizuri
-Inasaidia kuimarisha shina la nywele (hair strands/roots)
-Inasaidia kulainisha ngozi ya kichwa
-Husaidia kuweka balance ya mafuta kichwani (Natural scalp sebum)
-Inasaidia kupata usingizi vizuri , kupunguza uchovu na maumivu ya kichwa.

NB: Hakikisha unakua na utaratibu wa kufanya scalp massage kila unapopaka hair product yoyote au unapofanya treatment yoyote ya nywele angalau kwa dakika tano tu at least mara tatu kwa wiki. Hii inafanyika kwa wanawake, wanaume na watoto pia.

59. KUMBUKA: BIDHAA PEKEE HAZIKUZI NYWELE

Kitu ambacho watu wengi wanaotunza nywele wanatakiwa kujua ni bidhaa pekee haziwezi kukuza nywele, hata mtu anunue bidhaa za gharama kiasi gani lakini kama hazitunzi vizuri nywele zake na yeye mwenyewe hajitunzi kiusahihi (kulingana na matakwa ya ukuaji wa nywele) basi itakua ni kazi bure tu. Bidhaa za nywele hazikuzi nywele lakini zinachofanya ni kudumisha nywele zisikatike, kuzifanya ziwe imara, kusupport, kuzishika nywele vizuri wakati wa kustyle, kuzifanya zing'ae vizuri na kuchanika vizuri nk lakini nywele zinakua kutokea ndani.

Hivyo ili nywele ziweze kukua na kuwa ndefu lazima uzingatie vitu viwili vya muhimu;
1. Nywele zinazoota (New growth) ziwe na afya na kukutana na mazingira mazuri ya kichwa.
2. Kuzuia nywele zilizopo kukatika (Lengh Retention).

MAMBO YA MUHIMU YA KUJIFUNZA
Nywele zinatoka ndani ya fuvu la kichwa (scalp) hivyo kitu kinachopakwa nje hakiwezi kufanya nywele zikue sana au vizuri. Hivyo nywele zinahitaji chakula kutoka ndani kwa kufanya yafuatayo;
-Kula mlo kamili
-Kuepuka stress/msongo wa mawazo
-Kunywa maji ya kutosha
-Kutumia hair supplements
-Kupata muda wa kutosha kupumzika

-Bidhaa zinazopakwa nje zinasaidia tu kusupport nywele ziendelee vizuri lakini kinachofanya nywele zikue vizuri ni mwenendo wa maisha ya kila siku. Kitu cha muhimu zaidi ni kutunza ngozi ya kichwa maana ndio inayopokea nywele fresh kutoka ndani.

-Bila kusahau nywele inakua kwa 0.5-1.5inch kwa mwezi inategemea na genes za mtu (biologically), hiyo ndio iko hivo huwezi kufanya zikue haraka zaidi ila kinachotakiwa ni kuzitunza zile zilizopo ili zisikatike

NYWELE NZURI NI MATUNZO.