Tuesday, June 30, 2020

86. JINSI YA KUKUZA NYWELE KWA HARAKA


-Zifanye  nywele zako zisiwe kavu sana ( moisturize).

Tumia maji, moisturizing conditioner, au kwa kuchanganya nusu mafuta ya mzaituni (olive oil) na nusu mafuta ya nazi (coconut oil), au unaweza kutumia vyote kwa mpangilio sahihi.

-Fikiria kutumia protein conditioner. 
Hizi huzifanya nywele za aina flani kuwa imara na pia inaweza kuwa na madhara kwa kuzifanya nywele ziwe kavu na kukatika kiurahisi. usiiache kwenye nywele kwa muda lefu tumia kama ilivyo elekwezwa.

-Paka  mafuta mazito (to seal in moisture, kama vile Black castor oil or Shear butter)
Ngozi yako ya kichwa inapo kuwa kavu tumia mafuta ya nazi kupaka ngozi yako kwa kutumia ncha ya kidole chako. acha kupaka unapo kuta mba kwasababu mafuta hayo yanaweza kuwa chakula kizuri cha fangasi hao.Kama una mba paka mafuta mara  moja kwa wiki au tumia mafuta ya moto.

Pia tumia  neutralizing shampoo kuondoa  mafuta na madawa yote ulio tumia kwenye nywele zako.

NJIA YA PILI

-Tumia  vitamins
Vitamin supplements zinakupa virutubisho vinavyo kusaidia kukuza nywele zako


- Kula vyakula vya protein.
Vyakula vya protein kama vile nyama, maziwa, maharage ya soya, maparachichi, na mbegu za maboga.

Sunday, June 28, 2020

85. JINSI YA KUREFUSHA NYWELE KWA HARAKA

Kama wewe ni mwafrika au una asili ya afrika basi tambua kuwa nywele zetu hukuckua muda mrefu sana kurefuka. Lakini zipo njia zinazo weza kukusaidia kurefusha nywele zako kwa haraka. Leo tujifunze kidogo njia mojawapo ya kukuza nywele zako kwa haraka zaidi.

NJIA YA KWANZA
Kuosha na matibabu.

-Tambua aina ya nywele zako
Unaweza kutambua aina ya nywele zako kwa kuwaona wataalamu wa saloon, kujua aina ya nywele zako itakusaidia kuchagua matibabu sahihi na products  sahihi kulingana na nywele zako.

-Osha nywele zako pale tu inapo hitajika.
Usipende kuosha nywele zako mara kwa mara kwani unaziondolea mafuta ya asili. jaribu kuosha nywele zako mara moja kwa wiki au mara moja kwa wiki 2 kama huwa zinakatika katika.Tumia  shampoo ambayo haita zaicha nywele zako zikiwa kavu sana. Ili kupunguza  madhara ya bidhaa unazotumia zioshe  nywele zako kwenye maji ya vuguvugu kisha zisuuze kwenye maji yaliyo poa.

-Ziache  nywele zako zikauke zenyewe
Kama unatumia hair blower kukaushia nywele zako ni vyema utambue kwamba joto kutoka katika blower linaweza kukusababishia madhara katika nywele zako na kuzifanya zikatike kabla hazijafikia urefu unao uhitaji. Badala  yake unaweza kuzikusanya nywele zako na kuzifunga kitambaa na uziache zikauke usiku kucha, Au unaweza kuzikausha kwa kutumia taulo.
-Tumia conditioner kila  unapo osha nywele zako.
Shampoo inaondoa mafuta ya asili yaliyopo kwenye nywele zetu, badala yake unaweza kurudisha mafuta hayo kwa kutumia conditioner inayo faa kulingana na nywele zako.

-Paka mafuta ya nywele kila siku.
Ukipaka mafuta ya nywele unazifanya nywele zako ziwe laini  hii itakusaidia kuzuia zisikatike.
Tumia mafuta ya maji (kimiminika) kama vile;
🧚🏻‍♂️ Black castor oil
🧚🏻‍♂️Lavender oil
🧚🏻‍♂️Avocado oil
🧚🏻‍♂️Olive oil
🧚🏻‍♂️Coconut oil nk
Zifunge  nywele zako na kitambaa kuzisaidia zishike mafuta.

ITAENDELEA......

84. JINSI YA KUTUNZA NGOZI YA KICHWA

Mara nyingi tumekua tumeongelea jinsi ya kutunza nywele, leo tutaangalia  jinsi ya kuwa na ngozi ya kichwa yenye afya (Healthy Scalp)

πŸ€Nini ufanye ili uweze kumaintain ngozi yenye afya na kama ngozi yako ina afya ni rahisi nywele kuota vizuri na nywele kuwa na muonekano mzuri hivo msingi mzuri wa utunzaji wa nywele unaanzia kwenye ngozi yako  ya kichwa itunze vizuri sio kila mafuta unatumia unaharibu ngozi yako cha Kwanza,

NINI UFANYE
πŸ‘‰Kula vizuri na kunywa  maji kwa wingi
πŸ‘‰Epuka kuosha mara kwa mara nywele yako au mara chache wengine huosha mara moja hupelekea mrundikano wa uchafu.
πŸ‘‰Tumia  natural products (zisizo na viambata sumu) kwa nywele yako lakini pia unaponunua zingatia ingredients zillio tumika kutengenezea hizo products na muda wake wa kuisha (Expiry date)
πŸ‘‰Epuka  rangi za nywele na hata dawa za nywele zinadhoofisha sana nywele
πŸ‘‰Epuka  kusuka misuko hatarishi au kukazwa sana lakini pia massage kichwa chako mara kwa mara.


πŸ€Lakini pia kama unatatizo la miwasho mba wasioisha basi tumia steaming ya  tangawizi kitunguu swaumu na kitunguu maji saga pamoja unaweza changanya  na asali ukaweka kichwan kwa tumia hata mara 4 kwa miezi 2 (Hili somo lilishaelekezwa kwenye posts zilizopitaπŸ‘‰πŸ»πŸ‘‰πŸ»

πŸ€Au unaweza kuoshea apple cider vinegar unachanganya na maji vijiko viwili vya maji kwa kimoja cha apple cider vinegar (Hili pia lilishaelezewa)

πŸ€Pia unaweza kuosha nywele ukakata mistari kisha ukascrub kichwa chako kisha ukaosha tena hapa nazungumzia scrub ya sukari ukachanganya na mafuta ya castor oil  au scrub ya sukari, kahawa na asali unachanganya kisha ukascrub kichwani ukimaliza iyache ikae hata dakika 5 kisha osha. Scrub ni nzuri sana maan itasugua vzr mba watoke na inatibu miwasho kwa haraka pia hii njia sio steaming kwa nywele zako hivo unaweza ukaamua ufanye lini na ukitumia hii njia utatakiwa kuweka tena steaming kama kawaida.

Friday, June 26, 2020

83. JINSI YA KUTUNZA NYWELE ZENYE DAWA



Mara nyingi tumekua tukiongelea nywele za asili (Natural hair) lakini sio watu wote wenye passion (uvumilivu wa kutunza nywele za asili). Hivyo basi leo nitatoa tips kidogo kuhusiana na jinsi ya kutunza nywele zenye dawa (Relaxed hair) ili ziweze kupendeza vizuri.

Nywele zenye dawa ni nywele ambazo mwanzo zilikua za asili lakini zikaongezewa vilainishi (relaxers), hivyo kurudi kuwa natural kutoka kwenye nywele za dawa ni either ufanye transition (kuacha nywele ziotee huku ukipunguza zenye dawa juu) au kufanya big chop (kunyoa kabisa nywele zote na kuanza upya).

Tuangalie vitu vya msingi vya kuzingatia ili uwe na nywele nzuri zenye dawa
🧚🏻‍♂️Hakikisha unachagua dawa ya nywele inayoendana na nywele zako. Hapa pemdelea sana kutumia dawa za box na sio za kopo maana dawa za kopo ni kali mno zinaweza kuleta madhara ndani na nje ya kichwa ndani ya muda mfupi. Na dawa za nywele zinawekwa chini tutu kwenye maotea ya nywele usiweke juu.

🧚🏻‍♂️Lazima  upange muda wa kuweka nywele dawa. Dawa inatakiwa kuwekwa mara tatu au mbili tu kwa mwaka. Kama nywele zako ni laini basi unaweka kila baada ya miezi 6 na kama nywele zako ni ngumu sana basi kila baada ya miezi minne ndio unaweka dawa. Usiweke mara kwa mara; kumbuka hizo ni chemicals na zinaenda kukutana na ngozi ya kichwa directly. Pian wengine huweka dawa baada ya miezi mitatu vyote inategemea na aina ya nywele zako.

🧚🏻‍♂️Suka  mitindo rafiki na nywele zako usipende kusuka tu kila mtindo chagua mitindo ambayo haitakata nywele zako.

🧚🏻‍♂️Hakikisha  unaosha nywele zako mara  kwa mara. Angalau  mara  3 au nne kwa mwezi. Nywele zikijaa uchafu haziwezi kupumua vizuri hivyo zitakua kwa kusua sua sana.

🧚🏻‍♂️Tumia  mafuta rafiki na nywele zako. Mafuta  yenye uwezo wa kutunza unywevu na kuzuia nywele kukatika. Mafuta hayo ni kama vile Black castor oil, Coconut oil, Olive oil, jojoba oil nk

🧚🏻‍♂️Punguza  matumizi ya moto kwenye nywele..  Mfano .kupasi nywele au kukausha nywele na dryer. .Hii  hufanya nywele kutokuwa na nguvu hivyo kuwa dhaifu sana hivyo unashauriwa usifanye mara kwa mara.

🧚🏻‍♂️Tumia kofia ya satini au kitambaa cha safini wakati wa kulala (usilale kichwa wazi au na kitambaa kigumu); Hii inasaidia  nywele kufyonza mafuta ipasavyo na  kumaintain Ph

82. MAKOSA UNAYOFANYA WAKATI WA KUOSHA NYWELE ZAKO- PART 2



🧚🏻‍♂️Kutokuosha na kurudiaRinse & Repeat

Ni muhimu sana kuosha nywele na kurudia. Na hii ni muhimu zaidi kwa wale wenye nywele ndefu. Kama una nywele fupi au ndogo kabisa si lazima kwako kuosha na kurudia. Baada ya kuwa umesugua ngozi ya kichwa “scalp” kwa dakika tatu, ni muda wa kuosha nywele. Ukishaosha inafuata hatua ya pili ya uoshaji wa nywele. Unatumia shampoo kama kawaida. Kwenye hatua hii utaweka msisitizo zaidi kwenye nywele zenyewe kwakuwa tayari ngozi ya kichwa ulishashughulika nayo kabla. Mara hii weka msisitizo zaidi kwenye kuosha nywele zako na hakikisha hakuna nywele inayoachwa bila kupata shampoo kuanzia kwenye mzizi mpaka kwenye ncha.
🧚🏻‍♂️Kutokutoa  shampoo vizuri kwenye nywele.
Baada ya kurudia kuosha nywele kwa mara ya pili kinachofuata ni kutoa shampoo kwenye nywele.
Watu wengi hawatoi shampoo vizuri kwenye nywele, na hii huzifanya nywele kubaki na shampoo ambazo zinasababisha nywele kubaki na vitu vyeupe vyeupe “build-ups” na nywele pia kutosafishika vizuri. Hivyo inasisitizwa kutumia muda na maji ya kutosha kutoa shampoo na kuhakikisha imetoka kabisa kwenye nywele ili nywele zako ziwe zimesafishika vizuri.
Yapo makosa mengi sana ya utunzaji wa nywele yakianziwa na uoshaji wa nywele. Ila tukianza kuyasahihisha baadhi ya makosa tuliyoyaelezea hapo juu na kuanza kufuata utaratibu mzuri wa uoshaji wa nywele naamini sote tutakuwa tumeanza safari nzuri ya kuelekea kuwa na nywele nzuri na zenye afya!

81. MAKOSA UNAYOFANYA WAKATI WA KUOSHA NYWELE ZAKO-PART 1


Leo utajifunza namna sahihi ya kuosha nywele ili uziache nywele zako zikiwa safi kana kwamba umeziosha kwa mtaalamu wa saluni. 
Wote  tunaosha nywele ila haitakushangaza ukisikia kwamba uoshaji wa nywele zako si sahihi. Wengi wetu tumekuwa tukifanya makosa kadhaa wakati wa kuosha nywele. Baadhi yetu hatutumii muda wa kutosha kusugua scrub” ngozi ya kichwa “scalp”, hatuoshi vizuri na baadhi pia hatutumii conditioner. Na haya ni baadhi tu ya mambo ambayo tunakosea wakati wa kuosha nywele.

Yafuatayo ni makosa makubwa matano watu wengi huyafanya wakiwa wanaosha nywele
🧚🏻‍♂️Kutolowanisha nywele vizuri.
Watu wengi hawaloweshi nywele zao vizuri kabla ya kupaka shampoo. Ni muhimu kulowesha kila unywele kwa maji kabla ya kupaka shampoo. Kila nywele inahitaji kuloweshwa, kisha ipakwe shampoo ili ipate kutakata vizuri.
🧚🏻‍♂️Kutumia shampoo nyingi sana au kidogo sana.
Wote  tunafahamu kwamba kitu chochote kikizidi kina madhara au hakitaleta matokeo mazuri. Tunatakiwa kutumia kila kitu kwa kiasi. Si kwa wingi sana na si kwa uchache sana. Kanuni hii pia inatumika kwenye upimaji wa kiasi cha shampoo cha kutumia wakati wa kuosha nywele.
Kutumia shampoo nyingi kunaweza kukufanya usiweze kuipata nywele na kuisafisha vizuri kutokana na kuzidiwa na povu jingi sana. Na kutumia shampoo kidogo kutafanya nywele zako zisitakate vizuri. Pima shampoo kiganjani kwako, kiasi cha wastani kulingana na ukubwa na wingi wa nywele zako, kwa kutumia vidole paka shampoo kwenye nywele zako ulizozigawanya kwenye makundi manne. Paka kuanzia kwenye ngozi ya kichwa “scalp” kuja kwenye ncha ya nywele
🧚🏻‍♂️Kutotilia  maanani zaidi ngozi ya kichwa.
Kama  umeshawahi kufanyiwa shampoo kitaalam saluni bila shaka unajua ni muda kiasi gani huwa wanautumia kwenye ngozi ya kichwa. Kusugua ngozi ya kichwa ni hatua ya msingi zaidi kwenye mchakato wa kuosha nywele.
Watu wengi hawatumii muda wa kutosha kusugua ngozi zao za kichwa. Tunatakiwa kusugua ngozi zetu za kichwa kwa walau dakika tatu. Bila kujali urefu au aina ya nywele zako unachotakiwa ni kusugua ngozi yako ya kichwa. Na unatakiwa kufanya hivyo kwa kutumia vidole na sio kucha kwa muda usiopungua dakika tatu.

INAENDELEA....

Thursday, June 25, 2020

80. JINSI YA KUOSHA NYWELE


πŸ€Utaratibu wa kuosha nywele unaweza kuchangia nywele kukatika au kuto kukua vizuri hivo kabla sijaanza kufundisha steaming ni nini au protein ni nini basi tujifunze kuosha nywele zetu kwanza.

HATUA
🍫Step 1: Kama umesuka nywele fumua kisha detangle(kuachanisha vizuri kwa vidole ama chanuo pana)baada ya kuachanisha vizuri unaweza ku tumia detangle cream, spray au leave in conditioner( sio muhimu sana) kisha suka mabutu makubwa ama twist kama una nywele ndefu Kama una nywele fupi acha.

🍫Step 2:  apply mafuta ya kukuza nywele(growth oil) kama coconut oil, shime oil, , jojoba oil, castor oil, black seed oil, avocado oil au essential oil make sure ni kimiminika step hii inasaidia ngozi isikaukiwe na mafuta na ina act kama pree_poo(pree_shampooing) na unapaka zikiwa hivo zimesukwa.

🍫Step 3: osha kwa free sulphate shampoo hapa ziko nyingi inategemeana na brand gani utanunua osha vizuri ukiwa umezisuka kisha kausha kwa khanga au shati na kama utatumia taulo basi usisugue kalisha tu kichwani, pia kwenye kuosha waeza oshea maji ya vugu vugu kulingana na hair porosity yako.

🍫Step 4: weka steaming yako au protein treatment kulingana na ratiba yako vaa mfuko wa plastic kisha funga kiremba juu upate joto vizuri kama steaming yako ni ya saa moja,nusu saa au dakika 45 kaa mda huo  kisha toa, osha kwa maji ya baridi kisha kausha.

🍫Step 5: paka mafuta yako kisha paka leave in conditioner au paka leave in cinditioner( kama bamia,  alovera, flaxseed au za dukani nitakuja kufundisha) kisha mafuta.

🍫Step 6: suka nywele yoyote kama ya uzi au ya mkono, pia pendelea kulala na kitu kichwani hususani iwe na material ya satini.

79. JINSI YA KUFANYA NYWELE KUWA NA UNYEVU

Kama ambavyo mwili unahitaji maji kuendelea kunawiri vivyo hivyo nywele zetu zinahitaji unyevu ili kuendelea kuwa nzuri na zenye afya. Kuna niia ambazo zimezoeleka  kufanya nywele kuwa na unyevu; Hivyo wewe kama mtu unaetunza nywele unatakiwa ujue aina ya nywele zako na njia gani ya kuhifadhi nywele inkubalika na nywele zako.
Njia hizo zinaoneshwa vizuri kwenye picha hii πŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌ


C= Cream (Unaweza tumia Shea butter au  Mango butter)
O=Oil (Hapa tunatumia carrier oils kama vile Black Castor oil, Coconut oil, Olive oil, Jojoba oilnk)
L=Leav in Conditioner/Water based conditioner (Unaweza tumia ambayo inaendana na nywele zako, ila ambayo imezoeleka ni brand ya Cantu au Antie Jackies Leave in conditioners japo unaweza tumia ya asili ya kutengeneza mwenyewe nyumbani kama Vile Gelly ya Aloevera au ya bamia.

Wednesday, June 24, 2020

78. KANUNI 10 ZA KUWA NA NYWELE NZURI


🧚🏻‍♂️ Jua jinsi ya kuchana nywele zako kwa usahihi

🧚🏻‍♂️Jua jinsi ya kufumua nywele zako kiusahihi na jinsi ya kuzitunza wakati umefumua ili kuzuia kukatika.

🧚🏻‍♂️ Jinsi ya kubana na kusuka nywele pamoja na kuchagua mitindo rafiki kwa ajili ya nywele

🧚🏻‍♂️Treatments za  kufanya katika nywele zako
  - Steaming(deep conditioner)
  -Protein treatment
  -Hot Oil treatment
  -Hair mask
  -Leave in conditioner

🧚🏻‍♂️ Jinsi ya kupaka mafuta kichwani

🧚🏻‍♂️Vitu vya msingi vya kuwa navyo kabla haujaanza kuhudumia nywele zako

🧚🏻‍♂️Vitu vya kuepuka katika kuhudumia nywele zako

🧚🏻‍♂️Kwanini umeamua kuwa na nywele za asili

🧚🏻‍♂️ Una malengo gani na nywele zako

🧚🏻‍♂️UVUMILIVU

Tuesday, June 23, 2020

77. JINSI YA KUKUZA NYWELE KIRAHISI

Leo tuangalie mtu anawezaje kukuza nywele zake za asili kirahisi kabisa kwa kutumia vitu vya kawaida ambavyo vinapatikana jikoni kwa kila mtu.

MAHITAJI
-Kitunguu maji
-Tangawizi
-Kiazi mviringo
-Olive oil (Mafuta ya mzeituni)
-Mafuta ya nazi (Cococnut oil)
-Mafuta ya mnyonyo (Black Castor oil)
-Asali kidogo
-Kiazi mviringo

Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo husaidia kukuza nywele na kuzuia MBA kwenye nywele.

JINSI YA KUANDAA
 -Chukua kikwaruzio cha nyanya / karoti (grater) halafu chukua  kitunguu chako kwaruza pale upate ule uji uji wake
-Chukua tena tangawizi na kiazi kwaruza/kwangua upate ule uji uji baada ya hapo chukua chujio au kitambaa kisafi changanya huo mchanganyiko wako wote then chuja/kamua ili kupata juice  yake
-Ongeza vingine vyote vilivyobaki na uchanganye vizuri (mafuta unaweza kidogo kidogo tu)

NB: Unaweza kutumia blender kusaga vitu vyako vyote kwa pamoja halafu mwisho utachuja upate maji maji yake

JINSI YA KUTUMIA HUO MCHANGANYIKO WAKO
-Chukua chupa  weka hiyo juice iliyopatikana
-Funua nywele zako na uzipshe vizuri na shampoo isiyo na viambata sumu
-Paka  huo mchanganyiko wako kweny ngozi ya kichwa kwa kutumia vidole na sio kutumia kucha  paka kichwa mpaka kienee chote
-Chukua mfuko wa plastic au makofia   ya plastic vaa kichwan kwa muda wa saa moja au unaweza kulala nayo usiku kucha
(pia unaweza kukaa kwenye steamer kwa dakika 20 hadi 25 ili kupata joto vizuri)
-Baada ya hapo osha nywele zako vizuri na maji ya kawaida tu.

JINSI YA KUTUMIA MAFUTA
-Chukua mafuta ya nazi, ya mnyonyo na mzeituni kiasi kidogo changanya alafu yapashe kidogo yapate joto (Hot oil treatment)
- Paka vizur kwenye nywele kuanzia kwenye ngozi ya kichwa halafu kaa  lisaa limoja halafu osha  kwa kutumia shampoo hakika utazifurahia nywele zako.
-Mwisho paka mafuta yako ya joto la kawaida na hapo uko tayari kubana style yoyote au kwenda kusuka.

Friday, June 12, 2020

76. JINSI YA KUZUIA NYWELE ZAKO KUKATIKA

Henna ina matumizi mengi sana; leo tuangalie jinsi gani unaweza tumia henna kwa matokeo mazuri zaidi.
Leo tuangalie jinsi gani unaweza kutumia henna kuzuia nywele kukatika hasa ncha.

MAHITAJI
Vijiko vi 2-3 vya chakula vya henna
•Parachichi moja la wastani
•Yai moja (La kienyeji)
•Maji kidogo kama mchanganyiko utakua mzito sana

JINSI YA KUTUMIA
-Osha nywele zako vizuri na shampoo isiyo na viambata sumu
-Kausha kidogo nywele zako kuondoa maji yanayochuruzika
-Changanya vitu vyote upate uji mzito wastani, -Paka kichwani kuanzia kwenye ngozi mpaka ncha ya nywele zako. -Kaa na mchanganyiko huo angalau masaa mawili kisha osha.

KUJAZA NYWELE NA KUFANYA ZING’AE
MAJITAJI
•Chai ya rangi nusu kikombe
•Maji ya limao Kijiko cha chakula kimoja
•Yai au maziwa ya mgado

JINSI YA KUTUMIA
Loweka Henna usiku mzima kwenye chai ya rangi. asubuhi unapotaka kutumia ongezea viungo vilivyobakia. Paka dakika ishirini (20) Kabla ya kuoshwa nywele.

HENNA KWA AJILI YA NYWELE KAVU
Changanya Henna, mafuta ya nazi kiasi na Olive oil (mafuta ya mzaituni) uwe na uji mzito kiasi. Paka kichwani kaa nao lisaa kisha safisha.

NB: Hizi  treatment unaweza kufanya kwa nywele natural na zinye dawa, hakikisha unatumia Henna ya asili isiyotiwa kemikali.

Wednesday, June 10, 2020

75. JINSI YA KUTUMIA HENNA KAMA CONDITIONER

MAHITAJI
-Vijiko vinne vya chakula vya hena
-Nusu kikombe cha chai ya rangi iliyokolea majani
-kijiko kimoja cha chakula cha juice ya limao
-maziwa ya mgando (yogurt/mtindi)

JINSI YA KUTUMIA 
•Osha nywele zako vizuri kwa kutumia shampoo isiyo na viambata sumu
•Kausha nywele zako kidogo ili kuondoa maji yanayochuruzika
•Changanya vitu vyako vyote pamoja
•Paka mchanganyiko huo kichwani
•Kaa nao angalau lisaa.
•Baada ya hapo osha nywele zako na maji ya kawaida mengi
•Halafu unaweza fuata LOC Method kama kawaida.

Hii treatment italainisha nywele kwa maana ya kuzinyoosha na kuzipa mng'ao mzuri.

74. FAIDA ZA KUTUMIA HINA (HENNA) KWENYE NYWELE


Henna (Hina) inasaidia katika kubalance  hali ya kichwa kwa maana ya pH na kusaidia kuondoa muwasho wa ngozi ya kichwani.
•Inasaidia  nywele kukua kiusahihi
•Inapunguza  kukatika kwa nywele na kasi ya mvi kuota kwa wale wenye asili ya mvi au wenye umri mkubwa
•Inaweza kutumika kuzipa nywele zako rangi na mng'ao wa tofauti kadri unavyoitumia (Hair dye)
• Pia unawez  kuitumia Henna Kama conditioner (Tutaangalia kwenye somo linalofuata)

Tuesday, June 9, 2020

73. JINSI YA KUTUNZA NYWELE ASILIA (NATURAL HAIR)


Leo katika somo letu la urembo ningependa kuangalia katika utunzaji wa nywele bila ya kujihusisha na matumizi ya madawa ya kemikali ambayo yamesababisha kwa kiwango kikubwa matatizo katika ukuaji wa nywele kama nywele kukatika,kunyonyoka,kupooza katika ukuaji n.k

Hinw ni moja kati ya mimemq ambayo watu wengi hasa wanawake huitumia katika kujiremba hasa kujichora bila kutambua kuwa mmea huo unaweza tumika katika utunzaji wa nywele zao kwa kasi kubwa. Leo tutaangalia jinsi ya kutumia hina katika utunzaji wa nywele.

MAHITAJI
•Hina vijiko vitatu vya chakula
•Kipande cha ndimu au limao
•Maji ya chai kiasi kidogo
•Gloves mbili mpya

JINSI YA KUANDAA
Vaa gloves ili mikono yako isiharibiwe na hina
•Changanya hina na viungo vingine vyote hakikisha haiwi nyepesi sana wala nzito sana
•Gawa nywele zako katika mafungumanne, kisha paka hina yako kwa uangalifu, hakikisha kila fungu limekolea vizuri na usichafue uso wako
•Baada ya hapo unakaa nayo ukiwa umevaa mfuko wa plastic au kofia ya kulalia kwa muda usiopungua lisaa
•Zikiwa tayari unaosha nywele zako vizuri na kukausha kwa kitambaa cha cotton au tshirt
•Baada ya hapo unaweza kuziweka nywele zako katika mtindi wowote ule unaopenda baada ya kupaka mafuta mazuri yasiyo na chemicals (Black castor oil, jojoba oil, coconut oil or olive oil)

ITAENDELEA...
-Matumizi mbali mbali ya hina, kama vile kung’arisha nywele, kama stemaing, kukuza na kujaza nywele nk

72. MATUMIZI YA MLONGE KWENYE NYWELE


Mlonge ni mmea ambao unafaida nyingi sana katika mwili wa binadamu na unatumika sehemu mbalimbali duniani, hii inapelekea kuwa na majina mengi sana, baadhi nitayataja hapo chiniπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌ
✅Moringa Oleifera
✅Drumstick tree
✅Miracle tree
✅Ben oil tree
✅The horseradish tree
Na mengine mengi sana kulingana na eneo au nchi ambayo mtu yupo.
Mlinge unatumika katika bidhaa mbali mbali za afya na za nywele; Leo nitaongelea tu kuhusiana na umuhimu wake kwenye nywele.

Majani ya Mlonge (Moringa leaves) yanapendwa sana na watu wanaotunza nywele zao kwa sababu yana madini na vitamins za kutosha kurutubisha nywele vizuri.
Mlonge una;
•Vitamin A, E na B
•Calcium, Potassium, Zinc na Iron

FAIDA ZA MORINGA LEAVES
Yanaimarisha hair follicles
Yanaimarisha mzunguko wa damu, virutubisho na oxygen kwenye scalp
•Improve hair growing process (inasaidia ukuaji mzuri wa nywele)

JINSI YA KUANDAA
•Chukua majani kadhaa ya mlonge yaoshe vizuri yawe masafi
•Baada ya hapo weka kwenye sufuria, ongeza maji kidogo acha vichemke kwa muda wa dakika 5
•Acha maji yapoe, ongeza mafuta kidogo kisha uwe unaspray kwneye nywele mara kwa mara na baada ya kuspray seal in moisture.

Monday, June 8, 2020

71. MUAROBAINI (NEEM LEAVES) KWA AJILI YA NYWELE

Wote tunajua katika jamii zetu muarobaini/neem ni dawa nzuri sana ya asili, lakini leo sitakngelea kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali ya mwili; Ila nitaongelea jinsi gani muarobaini unaweza tumika katika kukuza nywele zetu (hasa nywele za asili).

FAIDA ZA MUAROBAINI KWENYW NYWELE
🧚🏻‍♂️Ni anti-bacterial; Na hii huenda kwenye scalp moja kwa moja hivyo inasababisha kupambana vyema na magonjwa nyemelezi ya kichwa kama vile mba, vidonda, kuwashwa nk.
🧚🏻‍♂️Inasaidia kuondoa infections mbalimbali kwenye kichwa kama zilikuepo na pia kulinda ngozi ya kichwa isipate infections kama haijawahi kupata.
🧚🏻‍♂️Kusaidia nywele kukua kirahisi na kiharaka zaidi, hata kama nywele zKo zilikua hazikui vizuri tumia muarobaini mara kwa mara utaona matokeo yake.

NB: Unaweza kupaka kwenye scalp tu au hata juu (kwenye nywele zote) ina nutrients za kutosha kunourish nywele zako vyema
Pia muarobaini una harufu kali kidogo hivyo kulingana na ulivyo unaweza chagua utumie kama leave in conditioner au kama steaming.

KAMA LEAVE IN CONDITIONER: 
-Unachukua majani kadhaa ya muarobaini, unayasafisha vizuri na kuyaweka kwenye sufuria
-Ongeza maji kiasi kama robo lita tu
-Acha ichemke kwa dakika 5 hivi ikiwa imefunikwa
-Baada ya hapo weka kando yapoe vizuri
-Halafu weka kwenye spray bottle yako, ongeza na mafuta kidogo kisha utakua unaspray kila ukihisi nywele kavu (wakati unataka kuzipa nywele unyevu)

KAMA STEAMING:
-Chukua majani kadhaa yasafishe vizuri
—Baada ya hapo weka kwenye blender ongeza na maji kisogo halafu saga
—Ukishasaga toa kwenye blender chuja na upate maji maji ya kijani
—Ongeza asali na mafuta yoyote ya nywele (Carrieer oils - mafuta ya mnyonyo, olive oil, coconut oil)
-—Nywele zikiwa safi paka mchanganyiko wako kwwnye nywele
—Unaweza  kucaa mfuko wa plastic, shower cap au ateamer kwa dk 30 hadi saa 1
—Baada ya hapo osha nywelw zako vizuri ili kuendelea na process nyingine kama vile LOC Method
-

Sunday, June 7, 2020

70. TUJIFUNZE ZAIDI KUHUSU DREADS (DREADLOCKS)


Dreadlocks, ni aina ya nywele ambayo ina historia kubwa kwa mwanadamu kabla ya style yoyote ya nywele, ni style inayotumika kiimani mfano imani ya Uhindi (Saddhus), Some of Tibetian Buddhists (Ngagpas of Tibet), Uyahudi (Nazarines peoples), Hamitic people of North Africa, Watakatifu wa Ethiopia na Oromos wa Ethiopia, Wasemitic, Wamisri wa zamani, Watakatifu wa Spartan wa ugiriki, na Kwenye uislam kuna wasufi wanaitwa Qalandariala (wana  natural dreadlocks) na Rastafarians (katika sects zote za Orthodox, Twelve tribes of Judah, Bobo Shanti na Spirituals). Pia kuachana na Imani imekuwa ni style kuonyesha jinsi unavyoheshimu nywele zako za asili (Your  natural hair)(Kwa Non-Africans and Africans)

Ushahidi wa kisaikolojia  wa kale unaonyesha aina hii ya nywele kiimani imeanza kutumika miaka kati ya 5000BC - 4500BC na ina umuhimu mkubwa  sana katika imani nyingi.

Kwa miaka ya sasa watu wamesahau heshima yake, ila wapo watu ambao wanapenda dreadlocks na wanazo, wanazitunza na kuzijali bila matatizo yoyote na wakiendelea kufanya shughuli zao za kimaendeleo (Sizungumzii wahuni wa mitaani). Pia wapo wengine wanazo kwa sababu ya Imani na wengine kwa sababu ya fashion.

TUTAENDELEA NA JINSI YA KUTUNZA DREADLOCKS


Monday, June 1, 2020

69. STEAMING NZURI KWA NYWELE ZISIZO NA DAWA

MAHITAJI
🧚‍♀️Parachichi 1 kubwa
🧚‍♀️Ndizi moja iliyoiva vizuri
🧚‍♀️Yai 1 la kienyeji
🧚🏻‍♂️Asali kijiko kimoja
🧚🏻‍♂️Mafuta (Castor oil, jojoba oil or coconut oil) kijiko kimoja

JINSI YA KUANDAA
-Andaa ndizi na parachichi vizuri kisha weka kwneye blender
-Saga vizor mpaka zilainike vizuri kuepuka kubaki na particles kichwani
-Ongeza asali, mafuta pamoja na yai kisha blend tena vizuri
-Baada ya hapo osha nywele zako vizuri na shampoo isiyo na viambata sumu
-Kausha nywele kidogo kuondoa maji yanayotiririka kisha paka steaming yako kuanzia chini kabisa ya nywele (kwenye shina) hadi juu
-Hakikisha nywele zote zimepata steaming
-Vaa kofia ya plastic (zile za kuogea) kwa dakika 45 au kaa kwenye steamer kwa dakika 20 tu. Hii inafanyika kuongeza joto ili steaming iweze kuingia vizuri kwenye nywele.
-Baada ya hapo osha vizuri na maji ya baridi (kufunga vitundu vilivyofunguliwa na joto)
-Halafu utaendelea na LOC Method kama kawaida

FAIDA ZA STEAMING HII
-Kulainisha nywele na kuzuia zisijifunge funge
-Kung’arisha nywele
-Ni chakula cha nywele hivyo kufanya nywele kukua vizuri
-Kuondoa mba, miwasho nk kwa sababu ya asali ambayo ni antifungus.

NB: Kwa matokeo mazuri fanya hii mara mbili kwa mweziπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

NYWELE NZURI NI MATUNZO